Kwanini Kenya wasitoke ICC peke yao?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Ningependa kuelimishwa hapa, ni kwa nini nchi ya Kenya inataka Bara zima la Afrika lijitoe ICC? Kama wao wanaona Mahakama hiyo haijawatendea haki ni kwa nini wao kama Kenya wasijitoe?
Ni kwanini wanataka Bara zima la Afrika lijitoe? Isitoshe Afrika siyo nchi moja na kila nchi inaingia mikataba kwa utashi wake yenyewe sasa kwanini kwenye kujitoa Kenya wanataka Afrika nzima ijitoe kwa kuwa tu wao wameshikwa?
 
Ndo nilichokuwa nasema kila siku siasa zao za ukabila sasa zinaenda continental! Na nchi za Afrika zisizojielewa zinashabikia nathani Tanzania inajua upuuzi wa hawa jamaa.

BTW wanajua wakijitoa ICC kuna uwezekano UNEP ikahama Kenya maana watapoteza eligibility to host a UN organ while against another UN organ
 
Kwa sababu ICC ime Base upande mmoja tu, kwa bara la Africa, wakati huko America kiongozi kama bush ni wa kupelekwa ICC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…