Kwanini kiinua mgongo "Terminal benefit" kikatwe kodi?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Wakuu kuna tatizo moja kwenye sera za Wizara ya Fedha kuhusu mafao kukatwa 40% ikiwa kodi ni 30% na NSSF,PSPF, PSSSF 10% kwa wanapewa mafao na kampuni zao baada ya kukatishwa mkataba ama kampuni kupunguza Wafanyakazi,hii ni kama ahsante kwa utumishi wao,ningependekeza hiyo hela wanayolipwa kana bakshishi isitozwe kodi maana mtu anaenda kuanza maisha mapya bila kazi.

Nafahamu kuwa hapa kuna vitu viwili tofauti.

1. Ni mafao ya Mfanyakazi NSSF ambayo alikuwa anachangia kila mwezi. Malipo haya yana utaratibu wake ambao ni wa kisheria kabisa na NSSF wanaufuata.

2. Kuna "kiinua mgongo" malipo ambayo MWAJIRI anamlipa mfanyakazi pale wanapoachana. Hii ni hiyari ya Mwajiri kulingana na makubaliano kati ya Mwajiri na Mwajiriwa.
Hapa tofauti ni kwamba ile ya kwanza NI KWA MUJIBU wa SHERIA.
Hii ya pili ni HIYARI ya Mwajiri kwa mujibu wa Makubaliano. Sasa hii ya pili, Kodi itahusika kwa ile HAND SHAKE Mwajiri anamlipa mfanyakazi wanapoachana,na hii inatozwa kodi mikononi mwa Mwajiriwa.

Sasa swali langu kwa watunga sera,kwa nini kiinua mgongo kitozwe kodi!?
 
Tupige kelele tuwe waumini wa kufuatilia michakato ya uundaji wa Sera katika wizara zetu ni mibovu mno. Lazima wataalamu ambao tupo nje ya mfumo tuongee ili kushinikiza marekebisho ya hizi Sera zinazoamliwa na wachache.y
 
Kelele zinasaidia tuendelee kupiga kelele 🤣🤣🤣.
Kelele huwapa nguvu viongozi kufanya maamuzi.Ni wajinga wachache wasioelewa umuhimu wa nguvu ya umma kwa viongozi.Kama ilivyo kwenye soka wakati mwingine kelele za washabiki huzisaidia club kufanya maamuzi.Angalia mwenendo wa Azam katika ligi pamoja na uwepo wa kila kitu lkn kwakukosa wapiga kelele imekua ikiyumbayumba tu.🤣🤣🤣
 
Wakuu kuna tatizo moja kwenye sera za Wizara ya Fedha kuhusu mafao kukatwa 40% ikiwa kodi ni 30% na NSSF,PSPF, PSSSF 10% kwa wanapewa mafao na kampuni zao baada ya kukatishwa mkataba ama kampuni kupunguza Wafanyakazi,hii ni kama ahsante kwa utumishi wao,ningependekeza hiyo hela wanayolipwa kana bakshishi isitozwe kodi maana mtu anaenda kuanza maisha mapya bila kazi.

Nafahamu kuwa hapa kuna vitu viwili tofauti.

1. Ni mafao ya Mfanyakazi NSSF ambayo alikuwa anachangia kila mwezi. Malipo haya yana utaratibu wake ambao ni wa kisheria kabisa na NSSF wanaufuata.

2. Kuna "kiinua mgongo" malipo ambayo MWAJIRI anamlipa mfanyakazi pale wanapoachana. Hii ni hiyari ya Mwajiri kulingana na makubaliano kati ya Mwajiri na Mwajiriwa.
Hapa tofauti ni kwamba ile ya kwanza NI KWA MUJIBU wa SHERIA.
Hii ya pili ni HIYARI ya Mwajiri kwa mujibu wa Makubaliano. Sasa hii ya pili, Kodi itahusika kwa ile HAND SHAKE Mwajiri anamlipa mfanyakazi wanapoachana,na hii inatozwa kodi mikononi mwa Mwajiriwa.

Sasa swali langu kwa watunga sera,kwa nini kiinua mgongo kitozwe kodi!?
Ni kwa sababu kodi yake haikuchukuliwa toka inakatwa. Suku zote PAYE hukokotolewa baada ya pension kukatwa. Na msingi wale ni kwamba mtu haja earn hiyo hela. Yaani bado hajanufaika nayo. Kwa hiyo siku akitaka kunufaika nayo ndio inakatwa kodi.
Hata hiyo ya handshake. Kimsingi unatakiwa kulipa kodi kwa fedha yoyote unayopokea. Hapo sasa ndio utajua wengi wetu ni watuhumiwa wa money laundering.
Ndio maana katika mifumo ya kodi inayofanya kazi sawa sawa, inaweza kutumika kuhalalisha utajiri wa mtu.
Kimsingi kila mtu anatakiwa kulipa kodi pale anaponufaika kifedha ndani ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom