Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Wakuu kuna tatizo moja kwenye sera za Wizara ya Fedha kuhusu mafao kukatwa 40% ikiwa kodi ni 30% na NSSF,PSPF, PSSSF 10% kwa wanapewa mafao na kampuni zao baada ya kukatishwa mkataba ama kampuni kupunguza Wafanyakazi,hii ni kama ahsante kwa utumishi wao,ningependekeza hiyo hela wanayolipwa kana bakshishi isitozwe kodi maana mtu anaenda kuanza maisha mapya bila kazi.
Nafahamu kuwa hapa kuna vitu viwili tofauti.
1. Ni mafao ya Mfanyakazi NSSF ambayo alikuwa anachangia kila mwezi. Malipo haya yana utaratibu wake ambao ni wa kisheria kabisa na NSSF wanaufuata.
2. Kuna "kiinua mgongo" malipo ambayo MWAJIRI anamlipa mfanyakazi pale wanapoachana. Hii ni hiyari ya Mwajiri kulingana na makubaliano kati ya Mwajiri na Mwajiriwa.
Hapa tofauti ni kwamba ile ya kwanza NI KWA MUJIBU wa SHERIA.
Hii ya pili ni HIYARI ya Mwajiri kwa mujibu wa Makubaliano. Sasa hii ya pili, Kodi itahusika kwa ile HAND SHAKE Mwajiri anamlipa mfanyakazi wanapoachana,na hii inatozwa kodi mikononi mwa Mwajiriwa.
Sasa swali langu kwa watunga sera,kwa nini kiinua mgongo kitozwe kodi!?