Kwanini kinaitwa Chama cha Mapinduzi? Ni mapinduzi gani kimeyafanya?

Kwanini kinaitwa Chama cha Mapinduzi? Ni mapinduzi gani kimeyafanya?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Hili swali najua wengi tumekuwa tukijiuliza bila kupata majibu sahihi.

Chama Cha Mapinduzi kiliundwa tarehe 05 February 1977 kutokana na kuunganishwa kwa vyama vikuu vya Tanu kwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar.

Mpaka hapo hatujaona mapinduzi yoyote kufanyika.

Kama kuna anayeweza kuelewesha nitashukuru
 
Ndio maana hicho chama hakina vision, bado wanajivunia mapinduzi ya Zanzibar mpaka leo, matokeo yake uchumi umewashinda kila kitu kimesimama na umasikini unaongezeka kila kona ya nchi, licha ya rasilimali za kila aina tulizonazo kama taifa.
 
Mapinduzi katika maendeleo.

CHADEMA inajiita Chama cha demokrasia na maendeleo lakini mwenyekiti ni wa kudumu na ofisi za chama zinapangishwa ufip
Kwani wapi CHADEMA imerudisha maendelwo nyuma? Kama Kila mtu atakuwa na nyumba na ofisi yake mwenyewe Ni kwamba real estate industry itakufa, Ni hasara kwa uchumi wa taifa kwani Land Lords ni registered tax payer.
Jina jingalao linasadifu utu wako wa ndani
 
Ndio maana hicho chama hakina vision, bado wanajivunia mapinduzi ya Zanzibar mpaka leo, matokeo yake uchumi umewashinda kila kitu kimesimama na umasikini unaongezeka kila kona ya nchi, licha ya rasilimali za kila aina tulizonazo kama taifa.
Inaumiza Sana kuwa na chama ongozi kinachoshindwa ku convert rasilimali zetu kuwa utajiri. Leo tunanunua yebiyebo kutoka Malawi na hata chipboard pia. Sera zetu za uwekezaji chini ya CCM ziko unstable kiasi kwamba badala ya kuchochea na kuvutia wawekezaji kinawakimbiza na kuwaogopesha
 
CCM wanasema kosa la KANU ilikuwa ni kukubali kuundwa kwa Katiba Mpya ya Kenya na ndiyo iliyowandoa madarakani...

CCM inasema, Mapinduzi daima..!!
 
Hilo ni jina tuu mkuu Bujibuji . Ni sawa na wale ndugu zetu wenye majina Kama Elihuruma au Godbless lakini unakuta ni majambazi. Mfano mwingine ni CDM, wanajiita chama Cha demokrasia na maendeleo Wakati Wana Mwenyekiti wa Maisha, hawapendi mtu anayechallenge fikra za mwenyekiti na hawana maendeleo zaidi ya kuwakamua graduates ambao ni jobless kwa kigezo Cha kuwatoa viongozi wa chama kwenye mahabusu mbalimbali nchini.
 
maana yake kutoka kwake inahitaji mapinduzi,siyo hivi hivi tu
 
Back
Top Bottom