Kwanini kipa namba 2 wa Simba Ally Salim haitwi Stars na badala yake anaitwa Benno Kakolanya ambaye ni kipa namba 3 wa Simba?

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Huu mpira wetu wa bongo una changamoto sana, leo kwenye mchezo wa Stars na Niger golini ameanza kipa namba tatu wa Simba Beno Kakolanya.

Halafu kipa namba 2 Ally Salim hata kufikiriwa kuitwa Stars imeshindikana, ingawa Ally Salim ndiye amedaka mechi zote za kumalizia msimu za Simba ikiwemo na Yanga na mechi kali na yenye tension kubwa dhidi ya Wydad Casablanca.

Kwanini Beno anakaa benchi Simba halafu Stars anaanza?

Kwanini Beno ni kipa namba 3 Simba lakn Stars ni kipa namba moja.

Kwanini Ally Salim hata benchi haitwi Stars lakini Simba anaaminika kupita Beno Kakolanya.

Viongozi wetu wana weledi wa soka kweli au mchezaji akidai maslahi imekula kwake?

Je Beno kudaiwa kujiunga na Singida Fountain ni sababu za kusoteshwa benchi Simba ili kiwango kife.

Sasa kwa mtaji huo kuna kipa mwingine hapa nchini wa kumnyima namba Beno Kakolanya ukiondoa Aish Manula.

Je, Simba hawaoni kumwachia Beno aondoke ni udhaifu wa hali ya juu kwao na watajuta?

Ngoja tuone
 
Mkuu Ally Salim sio kipa namba mbili Msimbazi Bali ni kipa namba 3,, sababu ya yeye kudaka mechi za mwisho za Simba ni kutokana na kipa namba 2 yaani Kakolanya kutokuwa na mahusiano mazuri na Simba ikisemekana anaweza kuifungisha makusudi.

Hata kama Kocha angekuwa mjinga kiasi gani asingeweza kumwita Ally Salim ,,

Pale Simba uswahili mwingi Sana mkuu.
 
Noted
 
Siku mkigundua uhuni wa Try again ndo mtakapovuka
 
Ally Salim sio kipa mzuri. Anabebwa na brand ya Simba. Anapenda kutema mipira. Angalia magoli aliyofungwa mechi ya Azam na Simba ndio utajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…