Kwanini Kisiwa cha Mafia sio sehemu ya Zanzibar?

Hadi uhuru Waingereza walitazama Kenya kisheria kuwa na sehemu mbili:
a) Protectorate of Kenya, yaani kanda la kilomita 16 (=maili 10) kwenye pwani la bahari, pamoja na visiwa vyote. Hili lilikuwa kanda ambalo waliwahi kukodi kutoka Sultani, wakiendelea kulipa kwenye makisio ya Zanzibar. Kisheria walitawala hapa kwa niaba ya Sultani.

b) Kenya colony, yaani maeneo yote mengine ya Kenya.

Hali halisi walitawala yote kama sehemu moja. Wakati wa uhuru wanasiasa wa Kenya bara hawakuwa tayari kutambua hali za Sultani, hivyo Waingereza walinyamaza tu na kukabidhi yote kwa serikali ya Nairobi. Hata hivyo, wenyeji wengine walipinga. Katika historia hii uko pia msingi wa mahakama za kadhi (mahakama za Kiislamu) zilizopo katika Kenya, maana Waingereza walitunza utaratibu waliokuta.
 
Umesimulia historia vizuri sana.
Niongeza mawili tu:
1) Ni kweli wenyeji wa Mafia husimulia hao Wasakalava wa Madagaska walivamia Kua kwenye kisiwa cha Juani (kisiwa cha pili cha Mafia) na kula watu wote. Ila tu hii ya kula watu tusichukue kama habari ya kihistoria. Wasakalava wako hadi leo pala Madagaska, hakuna uthibitisho kwamba walikula watu. Katika karne ya 18 walihofiwa kama watu waliovinda watumwa hadi Ngazija (Komoro) na kuwauza kwa Wafaransa na Waarabu. Kuna taarifa nyingi kuhusu shughuli hizi. Linganisha hapa Sakalava people - Wikipedia

2. Kuhusu Mafia na Zanzibar - unaongea kama wangepaswa kuchagua baina Tanganyika na Zanzibar. Hapa unataja Tangansika kama "Tanzania bara". Ila tu hii ni historia ya juzijuzi tu, si ya karne ya 19. Jina Tanganyika lilichaguliwa na Waingereza walipotafuta jina baada ya kutwaa koloni ya Wajerumani, mnamo 1920 hivi waliamua watumia "Tanganyika". Hadi kuja kwa Wajerumani kulikuwa na maeneo ya pwani (bila tofauti ya visiwa au "bara") yaliyokuwa chini ya Sultani na maeneo mengine ya ndani ambako Sultani hakuwa na athira; kisehemu nchi na maeneo ya kujitegemea (kama Usangu, Uhehe, nchi nyingi za Wachagga...) au sehemu bila serikali kuu ambako kila kijiji kilijitawala.

Ukiuliza je Mafia ingefaa kuwa pamoja na Zanzibar - basi swali hili ungeuliza pia kuhusu Tanga, Pangani, Saadani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Mikindani, LIndi . . . . maana sehemu hizo zilikjuwa sawa na Mafia hata kama si kisiwa.
 
HIVI HAKUNA NAMNA TUNAWEZA KUWA NA TANZANIA AMBAYO ZANZIBAR NI MIKOA KAMA BARA. IWE SERKALI MOJA, RAISI MMOJA! IKIBIDI ZANZIBAR IPEWE SPECIAL TREATMENT KATIKA HUDUMA KI MAISHA NA MIUNDOMBINU ILI WARIDHIKE. ITASAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA TANZANIA MAMA.
 
Nasema hivyo sababu mm ni mshirazi kutoka kisiwa cha mafia hila rafiki zangu wengi uniita mm mpemba na sina namna inabidi nikubaliane na hali

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Ni wachache sana kilwa waliochanganya...ila ni kweli historia..kwa mbali inawaweka karibu...lakini asilimia kubwa watu wa kilwa wanafanana sana na wa Tanganyika.. ...
 
huo utakuwa ni upumbavu kwa upande wa zanzibar, maana ni haki ya zanzibar kuwa nchi, wao ni sehemu ya muungano kwa hiyari. ila wao kama wao ni nchi kamili kabisa, ingekuwa muungano haukutokea, zanzibar ingebaki kuwapo na ingekuwa nchi jirani. na kwa vyovyote vile hawayokubali serikali yao ya kitaifa kufutwa na kiongozi wao hawatokubali aache kuitwa na kupambanuliwa kwa cheo na wadhifa wa urais
 
mbona tanganyika ilimezwa na zanzibar na hakuna anayepaparika? nionyeshe nchi ya Tanganyika! Ni kwa sabab watanganyika wanaelewa kuwa mipaka iliwekwa na binadam tena kwa maslahi yake ila undugu wetu uko pale pale. na hakuna asiyejua umoja ni nguvu. tukifuta mipaka manake tunarudi kwenye uhasilia na uhalisia wetu. hata mzanzibar anakuwa na nafasi kuwa rais wa Tanzania nzima kama anavyotokea wa geita au musoma au unguja. Nchi itaendeshwa kwa gharama nafuu. ubinafsi tu ndo watusumbua. mbona hushangai USA!
 
Umenena sana mkuu japo kimasikhara

Mambo kama sisi ni/sio taifa hayana mantiki sana ni kujitaabisha tu kidunia

Mimi naona hii iliyopo inaleta sana "Sisi/Wao"

Vunja Tanganyika, vunja Zanzibar mazima weka kitu kimoja

Mbona Mafia ni kisiwa lakini iko Bara

Zanzibar pia inaweza kuwa Bara

Lakini sasa utaratibu ukishafanyika hata hiyo bara haitakuwepo, itakuwa nchi mpja tu
 
Hakuna kitu kinaitwa zanzibar kuna Tanzania tuu
 
Naam naam
 
Sasa umeshasema dola ya kisultan... Usultan ulishaisha
 
Nakubaliana na mwandishi juu ya historia ya kisiwa cha Mafia, na kwamba Sultan alikuja kukiuza kwa Wajerumani, na kwamba kwenye Berlin Conference, Tanganyika iliangukia mikononi mwa mjerumani. Ila napata wasiwasi juu ya ulivojaribu kukitoa kisiwa hicho mikononi mwa mjerumani na kuja kwa Waingereza, na hasa unapohusisha mapigano ya Vita ya Kwanza ya Dunia

Kwa ufahamu wangu, baada ya kumalizika kwa WWI kulifanyika mkutano uliokuja na kitu kinaitwa Versailles' Treaty, ambao pamoja na mambo mengine, iliafikiwa kuwa mjerumani anyang'anywe makoloni mengi Africa, ikiwemo Tanganyika, na Tanganyika ikawekwa chini ya uangalizi wa Uingereza.

Na kwasababu tayari Mafia ilikuwa chini ya mjerumani, ambaye koloni lake la Tanganyika (ikihusisha Kisiwa cha Mafia) na kupewa mwingereza, ndivyo ambavyo kisiwa hicho kilivohama kutoka kwa mjerumani na kuja kuwa sehemu ya Tanganyika chini ya uangalizi wa mwingereza
 
Nini mafia? Hata unguja na pemba ni sehemu ya tanganyika isipokuwa kuna hulka imejijenga miongoni mwa watu wa visiwani kuwa wao ni waoman na washirazi kiasili ndio wenye nia ovu ya kutaka utaifa wao kando na tanganyika lkn ukweli usiopingika ardhi yote ya visiwani mali ya tanganyika. Kama hao machotara wanataka waende huko wanapojnasibu oman na iran lkn ardhi ni mali ya tanganyika hata kijiografia oman na iran wapi na wapi? Lkn tanganyika na visiwa vyote ni pua na mdomo ardhi yetu ya tanganyika haitaporwa kirahisi hivo mungu ibariki tanganyika
 
Mafia kweli ni kisiwa lakini si visiwa vyote viwe sehemu ya Zanzibar. Mafia iko karibu sana na Wilaya ya Kibiti kwa sasa, na kuna visiwa vingine kama Mbwera nk. Na usafiri wa kwenda Mafia ni rahisi sana kutokea Nyamisati ambayo ipi wilaya ya Kibiti (zamani ilikuwa wilaya ya Rufiji)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…