Kwanini kiswahili hakipo supported na biashara nyingi za mtandaoni?

Kwanini kiswahili hakipo supported na biashara nyingi za mtandaoni?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Ukiangalia kitu kama Kindle; biashara ya ebook ya amazon, hairuhusu uchapishaji wa vitabu vya kiswahili na hsli inakubali vitabu vya lugha nyingi ambazo ni ndogo kuliko kiswahili. Cheki hawa admob/adsense, hawakubali kufanya kazi na watu wenye content za kiswahili. Na hapo utashangaa wanasupport vilugha vidogo kabisa. Tatizo nini? Nini kifanyike?
 
Kiswahili kinatumiwa na mataifa machache sana Duniani hivyo ndio maana ni kazi kazi kukubalika.

Ila Lugha kama kingereza kipo worldwide hivyo ndio maana ni supported language
 
Kiswahili kinatumiwa na mataifa machache sana Duniani hivyo ndio maana ni kazi kazi kukubalika.

Ila Lugha kama kingereza kipo worldwide hivyo ndio maana ni supported language
mbona kuna lugha ndogo kuliko kiswahili. mfano kiswedish, kidenish nk
 
Harafu wanaangalia na mataifa mfano mataifa yanayo tumia Lugha kama hizo yapo vizuri kwenye online business ila Tanzania sisi bado sana na Kiswahili ni chetu tunamiliki.

Wewe juliulize nchi yetu hata kupokea pesa kutoka PayPal ni kisanga.
Swala sio kupokea pesa Kwa paypal maana AdSense hata hawalipi Kwa paypal ama lugha kuwa inatumiwa Sana ama la.

Google wanategemea matangazo kutengeneza pesa, wanazingatia idadi ya advertisers na advertisers wanapenda audience ipi.

Huku tz advertisers ni wachache Sana wanaonunua matangazo Google ads na advertisers wengi WA nje hawalengi nchi za Kiswahili Kwa sababu purchasing power ni ndogo Sana kama sio haipo Kwa baadhi ya vitu.

Ukitizama lugha ambazo AdSense inazikubali

Languages Google publisher products support - Google AdSense Help
Nchi hizo zina middle classes wengi na wafanyabiashara wengi wanaonunua matangazo ya Google ads

Ukitaka kupata picha, washa VPN kisha search Google best android phones, tazama page ngapi za matangazo zimeandikwa Ad.

Halafu zima VPN kisha search Google simu nzuri za android au best android phones halafu tazama kama utaona page yeyote imeandikwa ad.
 
Back
Top Bottom