Jana Mhe .Rais Samia alizindua Kitabu cha muongozo kwa Majaji na Mahakimu kinachohusu jinsi ya utoaji wa Haki za wanawake na watoto ktk kesi za mirathi ndoa na talaka n.k.
Sisi wananchi tunashukuru kwa hatua hiyo lakini tumeshangaa sana kuona kitabu hicho kuandikwa kwa lugha ya kizungu wakati haki zilizo andikwa ni za wananchi wa Tanzania ndio maana Mhe. Rais akasema kitafsiriwe haraka kwa lugha ya kiswahili, lkn swali la kujiuliza hawa waandisha wa kitabu hiki waliwalenga kina nani haswa? Watanzania au Wazungu?!
Hata kama walifadhiliwa na nchi hisani lkn haki zilizo kusudiwa ni za Watanzania hivyo ilikuwa ni lazima kitabu hicho kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili na sio kizungu.
Viongozi wetu haswa Muhimili wa mahakama acheni kuwahadaa Watanzania; kama kweli lengo lenu ni kutoa haki za Watanzania basi tumieni lugha ya Watanzania, acheni kuwafurahisha wageni na kuwaumiza Watanzania.
Haki za Watanzania lazima ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili