Kwanini kitengo cha Clearing and Forwarding kule TASAC kimefutwa na wale watumishi kuhamishiwa taasisi nyingine?

Kwanini kitengo cha Clearing and Forwarding kule TASAC kimefutwa na wale watumishi kuhamishiwa taasisi nyingine?

Kilamunu

Member
Joined
Aug 25, 2021
Posts
81
Reaction score
208
Najiuliza na kujiuliza tena na tena. TASAC palikuwa na kitengo cha Clearing and Forwarding ambapo hawa kazi yao ilikuwa ni kusimama kama serikali kufanya clearance ya kila kitu kutoka hapa nchini kabla ya kufanyiwa shipping mfano madini, mazao kama ngano, wanyama na vitu vingine sensitive ambavyo ndio tegemeo la fedha za kigeni kwa nchi yetu.

Sasa inakuwaje hichi kitengo kule TASAC kimefutwa na wale watumishi kuhamishiwa taasisi nyingine? Mana hawa watumishi wa Clearing and Forwarding chini ya TASAC walikuwa bega kwa bega na TRA na naamini walikuwa wanaokoa mapato mengi sana especially katika nyanja ya madini.

Kulikoni mwenye ujuzi anijuze mana roho inamuuma sana.Nlidhani kwa hali ilivo hao ndio wangewekewa mkazo na kuboreshwa sana.
 
Back
Top Bottom