KERO Kwanini Kituo cha Mafuta kilichojengwa Kimara Stop Over kimejengwa eneo la hifadhi ya barabara ya Morogoro?

KERO Kwanini Kituo cha Mafuta kilichojengwa Kimara Stop Over kimejengwa eneo la hifadhi ya barabara ya Morogoro?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Unapotokea mjini kwenda Mbezi, ukiwa eneo la KIMARA STOP OVER, kuna kituo cha mafuta kinachoitwa RUPIA.
Wakati wa Serikali ya awamu ya 5 nyumba nyingi na vituo vingi vya mafuta vilibomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara.

Mara tu Serikali ya awamu ya Sita ilipoingia tulishangaa kuona kituo kile kikianza kujengwa. Awali tulidhani ni cha Serikali, lakini kilipokamilika tukagundua ni cha mtu binafsi. Tunajiuliza:
  • Kwanini kikajengwa pale, katikati kabisa ya barabara mpya na ya zamani? yaani kituio kipo katikati ya barabara kuu na service road.?
 
Inakera kuona kuna mtu kapewa kibali cha kujenga kituo kipya cha mafuta eneo la hifadhi ya barabara pale KIMARA STOP OVER na amekipa jina la RUPEER. Tunajiuliza huyu ni nani? Karuhusiwa na nani? Mpaka kituo kifanye kazi kuna mamlaka kadhaa zinahusika.

Hizi mamlaka zilitoaje idhini? Kwa nini waliokuwa na vituo vilivyokuwa vinatoa huduma vilibomolewa kisha yeye kapewa kibali kujenga kituo kipya? Kwanini TANROADS wanalikalia hili kimya? Ni nani kawafunga midomo?

  • Kwa nini wananchi walipopiga kelele tukajibiwa TANROARD wanafuatilia na walipomaliza kufuatilia hatukupewa mrejesho?
  • Hivi ingekluwa enzi za hayati Magufuli wangejenga pale?
  • Nani hasa mmiliki wa kituo kile na alipata vipi kibali cha yeye kujenga wakati vilivyokuwepo vilibomolewa?
  • Kwa nini umma haujibiwi hoja hizi? Nini kinafichwa?
 
HIVI NI KWA NINI HII KERO HAIFUATILIWI?
INA MAANA HAKUNA ANAYEIONA ?
Hebu anayeweza, na hasa taasisi ya JF wawaulize TAKUKURU, huenda wakatupatia majibu. Wananchi tunataka kupata majibu.
Hawa ndio watu walioiweka serikali mifukoni mwao kwa ajili ya pesa zao ama umaarufu wao.
"Chura Kiziwi" yeye anawaangalia tuu.

HII HAIKUBALIKI.
 
Back
Top Bottom