Kwanini kodi ya sim kadi inapingwa

Kwanini kodi ya sim kadi inapingwa

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,335
Reaction score
6,186
Wanajf

nilipokua nasoma A level nilifundishwa maswala ya kodi walau kwa kiasi kidogo. Kuna principle of a good tax systemkama ifuatavyo

According to Adam Smith, Good Taxation System based upon the following Principles :

(1) Canon Equality or Benefit,(maana yake hiyo kodi inalipwa kulingana na uwezo wa mlipaji kwa maana rahisi tajiri analipa zaidi kuliko masikini na kodi hiyo iwanufaishe walipa kodi.)

(2) Canon of Certainty (maana yake mlipaji kodi anapaswa kufahali utaratibu mzima wa ulipaji wakodi husika bila usumbufu)

(3) Canon of Convenience (kodi hiyo isiwe inasababisha usumbufu kwa mlipaji kwa maana, lini, wapi na kiasi gani anatakiwa kulipa na ulipaji huo usimfanye ashindwe kupata huduma zingine za msingi)

(4) Canon Economy (maana yake kodi iwe rahisi kukusanya bila gharama kubwa kwa mkusanyaji na kodi hiyo isiwe kikwazo kwa maendeleo ya uchumi).

(5) Canon ofProductivity

(6) Canon of Elasticity

(7) Canon of Variety

(8) Canon of Simplicity

(9) Canon of Expediency

(10) Canon of Co-ordination.



Hizo nyinginemtu anaweza kujisomea. Kwa kuangali hizo principle nne zote kuna mgogoro mkubwa na ndio lengo la thread.


principle ya kwanza. Kodi ya simu masikini na tajiri tunalipa sawa bila kujali kipato au matumizi ya huduma husika hivyo kodi hiyo si kodi rafiki kwa mlipaji hata kidogo


haijulikani ni lini ama ni wakati gani mtu anachagiwa hicho kiasi kwenye simu yake. Mwanzo wa mwezi, katikati, kila siku ama mwisho wa mwezi? Je ikitokeza mpaka mwisho wa mwezi sijaweka muda wa maongezi nini kitatokea? Je kama ni kila siku je siku ambayo sijaweka salio itachukuliwa pale ninopoongeza salio? N.k haya yote hayajulikani kwa mwanachi na hakuna uwazi kwa jambo hili linavyofanyika.


Convinience: lipaji alinunua handset alilipia kodi, mlipaji alinunua simcard alilipia kodi, mlipaji analipa kodi ya VAT kwa kila dakika anayotumia. Ili aendelee kuichangia serikali kodi ya ongezeko la thamani lazima aendelee kutumia simcrd, je
kuna uhalali we kulipia simu kadi? Mbona hatulipii tv, fridge, home theatre music system etc why simu. Hii kodi siyo convinient kwa mlipaji

Mkusaji TRA hajui kwa uhakika ni kiasi gani kinapaswa na kwa hakika kitakusanywa na makmpuni ya simu, hana mfumo wa kutrack active simcard na wanaokusanya kodi hiyo ni makampuni ya simu kwa niaba ya TRA. Kama wameshindwa kukusanya VAT na kodi nyingine za mapato wataweza hizi simcard? Vinginevyo wanahitaji kutumia gharama kubwa kufunga mitambo ya kutrack active simu card kila mwezi ili kujiridhisha ni simcard ngapi zimelipa monthly tax. Lakini wakusanyaji Aggregator ambao ni kampuni za simu wanatumia gharama kuzikusanya je hawatumia gharama zaidi ya 10percent ? Kuna watu watacha kutumia simu zao kwa sababu hawana uwezo wa kulipa hizo sh elfu moja kwa hivyo tayari kuna athari kiuchumi.


Kwa vigezo hivi vichahce nasema kodi hii haifai




Karibu kwa mjadal
 
Nadhani sababu kubwa ni kwamba hiyo kodi inawagusa moja kwa moja na kwa uwazi kabisa wananchi (wapiga kura) walio wengi hivyo Serikali haiwezi ku-afford uwepo wa beef la hivyo kati yake na majority, wapinzani wameseize opportunity hiyo na kuanzisha ligi kati ya serikali na wananchi walio wengi, Kwa serikali inayoishi kwa njia za kuwafisadi wananchi kwa mlango wa nyuma, lazima ipige magoti katika hili. Siwezi kufikiria sababu genuine zaidi kwa serikali kula matapishi yake katika hili:embarrassed1: kwa sababu serikali haiwezi kuchukulia hoja za wapinzani in good faith hii ni moja ya njia chache zilizobakia kwa upinzani kuibana serikali hii ya wacheza kiduku.
 
Back
Top Bottom