econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Nashangaa sana wazee wa mwanzoni akina Mtei na Makani walifanya uenyekiti wa CHADEMA kama nafasi huru hawakutaka kukaa madarakani mpaka waondolewe kwa nguvu. Kwa Sasa ni CHADEMA imejenga mtindo wa kwamba akitokea kiongozi mwenye ushawishi akagombea uenyekiti wa chama huwa anageukwa na kuitwa msalaiti.
Mifano ni mingi Sana:
1. Kuna chaha wangwe, huyu hadi alisimamishwa chama, kutokana na kuwa na msimamo mkali dhidi ya mwenyekiti na kutaja hadharani angependa awe yeye mwenyekiti wa chama.
2. Kuna Zitto Kabwe naye alipojaribu alizuiliwa na kuitwa majina mengi na hata baadae kuhama chama.
3. Kuna Kansa Mbaruk, alipojaribu alikutana na kigingi mpaka alipohamia ACT.
4. Kuna Sumaye, yeye alipojaribu aliambiwa sumu haionjwi kwa kulamba. Ikabidi arudi CCM alikotokea.
5. Kwa Sasa tunaye Tundu Lissu, yeye kashatangaza kugombea uenyekiti wa CHADEMA na kashachukua na kurejesha fomu ya uenyekiti. Ila amepata mashambulizi mengi Sana. Mara anatumika na CCM , mara anafadhiliwa na CCM akiharibu chama, mara ni kirusi ndani ya CHADEMA etc. Leo Lissu anatukanwa kisa tu kachukua fomu ya uenyekiti. Bila fomu ya uenyekiti Leo hakuna mtu angemsema Lissu vibaya.
Najiuliza swali moja kubwa, je ni dhambi kugombea uenyekiti CHADEMA? Kama ni dhambi iandikwe kwenye Katiba kwamba mpaka Mbowe afe ndipo watu wenye ushawishi kwenye chama watagombea Uenyekiti. Leo Lissu amekuwa shetani kwa kuchukua fomu ya uenyekiti, Leo Lissu anazodolewa na Wana CHADEMA kisa kachukua fomu ya kugombea uenyekiti.
Inasikitisha sana, Kwa chama kama CHADEMA kinahangaika kuutukuza ufalme na kutokupokezana uongozi.
Inasikitisha sana.