Kwanini kugombea Uenyekiti CHADEMA ni dhambi?

Kama na wewe uko kama mimi hujui mambo yaliyo chunguni, wanajua wao. Kuna jamaa mmoja alimpiga mkewe na kumtishia kumuua kwa bastola (nilivyosikia). Mke wake ni mwanasheria mwandamizi wa serikali. Kesho yake, mkewe akaleta gari likapakia mizigo yake yote, then off she went. Majirani walijitahidi kusuluhisha wapi. Kilichofuata ni divorce mahakamani. Yaani jitihada za majirani, ndugu na marafiki kuwasuluhisha ziligonga mwamba. Sisi pia tulitamani Chadema waendelee kuwa wamoja, lakini wao wanajua zaidi tatizo kuliko sisi. Acha wanyukane, na kama ulivyomsemo wa kabila letu "anayemwoa mama ndiye baba", basi atakayeshinda Kwa wingi wa kura ndiye atakayekuwa mwenyekiti wa chama chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…