1. Nianze hoja kwa kuomba wahusika na wadau wa idara, kurugenzi na wizara wafanye uchunguzi ili wajiridhishe na kuthibitisha uhalisia wa swali hili.
2. Lengo la serikali kuwapa watumishi wake fursa ya kujiendeleza kimasomo (mafunzo kazini) ni kuweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi na hatimaye kuleta tija stahiki kwa serikali na umma kuwa ujumla.
3. Pamoja na malengo hayo tumeshuhudia mara nyingi na kwa wingi walimu wengi wakipata fursa ya kujiendeleza na hivi sasa yawezekana kuwa tunao walimu wengi hasa wa shule ya msingi walio na kiwango cha shahada na kwa takribani karibu walimu wote Wana kiwango cha stashahada.
3. Hoja ni ipi? Mwalimu anapokwenda masomoni kwa maana ya mafunzo kazini ni matarajio makubwa kuwa akirudi atakuwa na mbinu mpya za kiutendaji Katika kile alichokwenda kuongeza ujuzi ila kwa sasa imekuwa kinyume chake, maana akirudi hata zile mbinu zake za awali anakuwa amezisahau na pengine hata ujuzi anaorudi nao unakuwa hauna nafasi katika kazi yake ya msingi, na hili hutokea Sana kwa walimu wa shule ya msingi.
4. Maoni yangu ni kwamba kuna haja ya kupitia aina ya mafunzo yanayolenga mafunzo kazini ili yalenge kuboresha mbinu na kuongeza ujuzi wa juu na ulio bora wa somo lilelile alilokuwa akifundisha kuliko kufundishwa kozi ambazo pengine ni mpya na haziwezi kutumika katika kazi yake.
5. Hapo nyuma tuliona kilianzishwa chuo cha stashahada ya ualimu kwa shule za msingi, kwa muda mfupi nilioshuhudia wahitimu wake walikuwa wameongeza kitu kipya na bora kilichoweza kutumika katika masomo yao.
Ni vizuri wangeweza kuboresha zaidi kuliko kuifuta stashahada hiyo na kulazimisha kila mwalimu awe na stashahada ya sekondari.
Ni kweli kwa sasa walimu karibu wote Wana stashahada ya sekondari lakini matumizi yake ni sawa na bure.
Karibuni kwa mjadala.