Kwanini kuku wanataga sehemu moja? Msaada jamani

Kwanini kuku wanataga sehemu moja? Msaada jamani

ayunus

Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji sasaivi wamefika mia na hamsini tatizo wanataga sehemu moja wnalalia sehemoja wa tatu kila siku wanachanganya mayai matokeo yake wanayaharibu tu msaada tafadhali.
 
Unachotakiwa kufanya ni kuwaandalia mazingira rafiki ya kutagia, yaani humo ndani ya banda jenga kama viota wanapenda.
 
Tenga viota vya kufanana na katika kila kiota weka yai moja ama mawili
 
Kuku hupenda kutaga sehemu iliyo jificha kidogo, kwa hiyo si ajabu hapo kwenye hicho kiota wanapongangania pamejificha kuliko viota vingine. Pia jaribu kuongeza idad ya viota" kwa kuku 150 ingelbid walau uwe na viota 75. Vile vile kuhusu kuchanganya mayai nunua mark pen na uyawekee alama yale ya kuatamiwa halafu yatakayo ongezeka au kuku wakiyachanganya itakuwa rahis kwako kuyajua na kuyatoa. Kaz njema.
 
Back
Top Bottom