matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Watu wa dini, wasioamini Mungu, freemasons kupitia charity zao, wote wanaunganishwa katika jambo moja la kutoa msaada kwa watu wenye shida.
Kutoa kwa kusukumwa na huruma kwa mwanadamu mwenzako ni ibada kamili iliyokamilika. Hii kazi ilipaswa kufanywa na Mungu mwenyewe aliyemuumba huyo mtu, wewe kuingilia kati ni kuamua kishirikiana na Mungu kufanya jambo la kiungu.
Kutoa msaada kwa kusukumwa na sifa binafsi, kupata umaarufu au kuwapiga chenga watu kuficha uovu wako kwa kuhamisha malengo ni ibada binafsi ambazo anayeabudiwa hapo ni wewe na waliokusukuma qu kinachokusukuma kufanya hivyo.
Ufanye nini sasa.
Hakikisha unatoa msaada ukisukumwa na huruma bila kuwa na nia kificho au faida binafsi katika msaada huo. Hiyo ni ibada kwa Mungu na atakufanya kuwa mfereji wa kupitishia utajiri wake ili watu wengi wanufaike.
Ni hilo tu