Utafananishaje Act wazalendo na Chadema? Chadema wameshindwa hata kujenga ofisi zao ndio utawafananisha na ACT wenye ofisi za Hadhi kubwa kuweza kufanyia vikao vyao? Ruzuku za chadema mpaka leo haijawahi kueleweka zinakwenda wapi lakini ya Act wazalendo imeonekana kazi yake ndani ya muda mfupi. Chadema Nafasi ya Mwenyekiti Ni ya urithi na haitakiwi mwingine yoyote kuitamani Wala kuigusa maana huko ni sawa na kuonja sumu wakati Act wazalendo wanagombea bila kutishiwa na kuitwa msaliti
Wewe ni mgeni Sana humu jf ila unapenda kurukia mambo. Ufanyie kazi ushauri uliopewa na Pascal Mayalla.
1. Kwanza, lazima ujue ACT ni chama kilichotokana na mgawanyiko CHADEMA baada ya kuondoka kwa Zitto Kabwe na Wenzake akina Prof. Mkumbo. Na baadae kikapata nguvu baada ya Maalim Seif kuhama CUF. Hivyo hicho chama ni waliohama CHADEMA na CUF.
2. Pili, hiyo ofisi ilikuwa ya kambi ya Maalim Seif ndani ya CUF baada ya kunyanganywa ofisi za buguruni na msajili wa vyama vya siasa. Hivyo Maalim Seif alipohamia ACT akahamisha na hiyo ofisi yake. Sio akina Zitto walioijenga, wao wamemalizia ukarabati.
3. Tatu, CHADEMA kwa sasa haipokei Ruzuku, na ndio chama pekee ambacho hakijawahi kupata hati chafu kwenye mahesabu yao ukiondoa kasoro ndogo zilibainishwa na CAG.
4. Nnne, Mwenyekiti sio wa kurithi Bali huchaguliwa na wanachama. Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA alikuwa Mtei, akamuachia Bob Makani na Makani akamuachia Mbowe. Kumbuka mwaka 97 na kuendelea Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema na mwaka 2000 alikuwa mbunge wa Hai na 2005 akapitishwa kugombea urais. Kipindi hicho CHADEMA haina nguvu Kama leo, lakini Mbowe akakiweka kwenye limelight kwa jinsi alivyoendesha kampeni zake mwaka 2005. Kwanza kwa kutumia helcopter, pili, kwa kuvaa combat ,tatu kwa kutumia msemo wake wa people's power na nne hoja zake zilikuwa na nguvu Sana. Kuanzia Hapo 2005 CHADEMA ilianza kupata jina na ufuasi mkubwa bara.
Mbowe amepata back kubwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA muda mrefu maana ndio ameleta mageuzi CHADEMA na kuinfluence watu wengi kuhamia CHADEMA. Zitto na unafiki wake anakiri Mbowe ndio aliyemuinpire kuingia CHADEMA kwa kumtembelea UDSM na kumshawishi awaingize vijana wengi CHADEMA. Kutokana kuinfluence watu wengi ndio maana ameendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa muda mrefu.
5. Tano, nakushauri, kabla hujaongea kitu fanya utafiti. Usiongee tu kisa unajisikia kuongea , ipo siku utaulizwa kwa nini uliongea hivyo utakosa majibu.