Kwanini kwasasa wanawake wengi wamekuwa hawana huruma na malengo mema kwa waume zao

Kwanini kwasasa wanawake wengi wamekuwa hawana huruma na malengo mema kwa waume zao

0ozg Tz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
4,155
Reaction score
11,168
Kwasasa usitegemee mwanamke anaweza kukuonea huruma wewe mume wake, haijalishi unapambana vipi kwa ajili ya familia yako, anytime anaweza kukufanyia tukio la hatari.

Kwasasa hawa viumbe tuliozoea kuamini kuwa wana huruma, huruma wamebakiza kwa watoto wao na kwa ndugu zao wa damu tu.

Sometimes nawaza labda mienendo yetu sie wanaume ndio imewabadilisha hivi, yale mambo yetu ya kuwanyanyasa, kufanya mambo bila kuwashirikisha, usaliti na mengine mengi.

Haya ni mambo ambayo kwasasa wanawake wanatufanyia wanaume bila kuwa na hata chembe ya huruma hata majuto hawana:-
* Mwanamke anazaa nje ya ndoa,unapambana kuhakikisha watoto wanasoma unapgwa mvua na jua na bado mwanamke anakuwa anakuchanganya kwa inshu za ajabu ajabu pasipo hata kuwaza kuwa huyu mtu anahangaika kusomesha damu zingine zisizokuwa zake ni heri nimpeleke taratibu,hilo hawa viumbe hawana.

* Mwanamke anapoona watoto wamekuwa wakubwa wanaweza kujitegemea na kumtumia vihela yeye, basi mumewe waliezeeshana anaanza kumuona sio lolote, Mara hataki tena kukaa kwake anaenda kwa vijana wake.

* Upo mihangaiko unarudi nyumbani unakuta mke kabeba kila kitu ndani kasepa, wakati hivyo vitu kuvipata umetumia takiribani miaka 3.
 
Ukatili katika jamii umeongezeka kwa sababu majeraha yamekuwa ni mengi. Wanawake wamekuwa victims wa uovu mwingi kupelekea kuzaliwa kwa usugu katika mioyo yao. Sasa ile huzuni na maumivu huzaa ukaidi ambao hauna point of return.

Mwanamke yeyote ambaye ana mambo ya kikatili chunguza historia yake anayo painful past ambayo pengine imetengenezwa na mwanaume au mwanamke mwenzake. Yote Haya hupelekea mambo unayozungumzia kufanyika. Uonevu, vipigo,

dharau,mateso.....usitegemee vikazaa utu wema....lazima huruma ife kwa mambo haya
 
Wametoka kwenye ubavu wetu ila nowdays wametuzidi Sana, utandawazi ni shida sana, Mfumo dume hauepukiki kikubwa kuwa na akili tu,usipige,usitukane Wala usiue, kaa kimya KARMA inafanya kaz kimyakimya.
 
Afadhali huyo nakwambia mwingine anaroga kabisaa ufukuzwe kazi!!
 
Cha mno !! Dunia kwa sasa ni tofauti hkn haja ya kumvumilia mtu atakaye kukimbia pindi mkizeeka!! wewe chapa tambaa au tafuta wenye hela haswaa oa hao!! lkn hawa wakutegemea mara apate kazi sijui anitunze maweeee!! utachakaa!!

Weka mijengo yako maalum mahali , pangisha kula cha juu!! hawa wa kukimbiwa nimeona wengi sana, mke ana change hata nyumba yako inakuwa yake!!
 
Mke wako anapanga ufukuzwe kazi!,afu maisha yaweje,duh!?
Wengine wanadanganywa na maadui zako, wale wenye kijicho na kipato chako, hata rafiki yako, Shangazi yako, jirani hapo ni mpaka mwanaume uwe na akili sana, hata ukiharibikiwa hajui ni zile dawa yaani mke kwa dunia ya leo uwe makini sana nae!
 
Kuna rafiki yangu kamwonea huruma mume wake kakopa kamnunulia kibajaji ...mume tukaz hutu TWA sikuiz kilasiku kupunguza wafanyakaz.Bwana wee,si mume kanyata usiku kakibebelea kibajaji jujuu kasepa jumla kasahau na watoto
 
Back
Top Bottom