Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Kati Mashahidi wote waliotajwa na Jamhuri hakuna shahidi ambaye alishuhudia upekuzi nyumbani kwa watuhumiwa. Mara nyingi upekuzi unapofanyika viongozi wa serikali ya mtaa ushiriki na utumika mahakamani kuthibitisha kwamba vielelezo vilivyokutwa kwa mtuhumiwa ni sahihi kwa uelewa wake.
Katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake Mashahidi wengi Ni Watumishi wa umma ambao wanatoka kwenye dola. Lakini hati ya mashtaka na vielelezo vinaonyesha kulifanyika upekuzi nyumbani kwa watuhumiwa, kwakuwa Polisi wanaonekana walikuwa well informed kabla ya arrest na upekuzi walishindwa Nini kushirikisha viongozi wa eneo husika au hata majirani kuonyesha kweli kwamba uniforms za Jeshi na vitu vingine vimekutwa kwa watuhumiwa?
Nakumbuka kesi ya mdude ilikuwa na elements Kama hizi ambapo huoni shahidi nje ya Polisi na dola kwenye mchakato wa uchunguzi. Hati ya upekuzi inasainiwa na mtuhumiwa labda na mke wake ambapo tunaelewa wazi kwamba mke awezi kumtolea ushahidi wakumfunga mmewe hasa kwa kesi asiyo na maslahi nayo. Lakini pia zipo kesi nyingi ambazo tuhuma uelekezwa kwa Jamhuri kwamba vielelezo walikwenda navyo kwa mtuhumiwa na wanapotakiwa kuthibitisha ushindwa.
Je, Hali hii yakukosekana independent witness ilitokea kimakosa au ilifanywa kwa kiburi kwamba mtu anaweza akafanya afanyavyo nakupeleka mahakamani?
Sehemu nyingine Ni pale unapogundua Mbowe alipohojiwa hakukuwepo mwanasheria wake na hapa unakutana na maelezo mahakamani kwamba watuhumiwa wanayakana maelezo yao means hata maelezo yaliyofikishwa mahakamani Yana utata na mjadala. Kwanini kesi nyeti Kama hii inakosa ladha ya professionalism? Maana hata Kama nimaelekezo Kama watu wanavyosema Basi ionekane consistency ya ideas,facts na elements.