Kwanini kwenye Matukio ya Kiserikali Viongozi wa Dini hufanya maombi kwa kusoma karatasi kama risala?

Kwanini kwenye Matukio ya Kiserikali Viongozi wa Dini hufanya maombi kwa kusoma karatasi kama risala?

tamsana

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
3,739
Reaction score
8,044
Salam!

Nimekuwa najiuliza maswali kuhusu wanachofanya viongozi wa Dini wanapoalikwa kwenye matukio makubwa ya kitaifa hasa yanayomuhusisha Mhe. Rais.

Moja ya swali ninalojiuliza ni namna viongozi hao wanavyofanya SALA/MAOMBI kwa kusoma kama wanasoma risala.

Nauliza ndio utaratibu wa serikali au lazima wanachoenda kuomba kihaririwe na mamlaka za Rais zinazohusika? Nimeuliza maana sio utaratibu kwenye nyumba zetu za ibada kiongozi kusoma maombi kama anasoma biblia.
 
Kwahiyo ulitaka wakamuumbue hangaya hadharani kwa kigezo cha sala ama? Watawala wengi ni wapuuzi sana na wana mafigisu kibao kuachilia mambo yafanyike tu ni balaa anaweza akajitokeza kiongozi anajiita wa dini ila akachafua hali ya hewa na ikumbukwe kwenye sala hamna wakukuzuia hadi umalize.
 
kwahiyo ulitaka wakamuumbue hangaya hadharani kwa kigezo cha sala ama? watawala wengi ni wapuuzi sana na wana mafigisu kibao kuachilia mambo yafanyike tu ni balaa anaweza akajitokeza kiongozi anajiita wa dini ila akachafua hali ya hewa na ikumbukwe kwenye sala hamna wakukuzuia hadi umalize .
Kama ni hivyo hakuna haja ya kualikwa hao viongozi. Tutawaombea viongozi wa serikali kwenye nyumba zetu za ibada inatosha kabisa.
 
Ninavyoona mimi;

Ni ili wasijisahau wakaanza kuhubiri na 'kunena kwa lugha'

Na pia kupangilia muda vizuri(pacing) kwa sababu ni rahisi zaidi mtu kuwasilisha hotuba kwa muda mfupi, ikiwa amepewa maneno machache,
kuliko kutengewa muda halafu abuni maneno yake mwenyewe, atazidisha muda
 
Ni lazima wahakiki, mf. "Ee Mungu mwangazie huyu mpumbavu ili aache kunyanyasa watu".hiyo ni sala yenye tusi ndani, inapashwa irekebishwe.
 
Ninavyoona mimi;

Ni ili wasijisahau wakaanza kuhubiri na 'kunena kwa lugha'

Na pia kupangilia muda vizuri(pacing) kwa sababu ni rahisi zaidi mtu kuwasilisha hotuba kwa muda mfupi, ikiwa amepewa maneno machache,
kuliko kutengewa muda halafu abuni maneno yake mwenyewe, atazidisha muda
Maombi na sala nzuri ni zile tunazowaombea kwenye nyumba zetu za ibada. Huko kwenye matukio ni kuonesha tu kuwa wanawashirikisha.
 
Back
Top Bottom