Kwanini kwenye sheria wanapenda kutumia kilatini na Kifaransa?

Vicin

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2017
Posts
676
Reaction score
295
Habarini wadau.
Kuna lugha nyingi sana duniani, lakini kwanini kwenye sheria utakuta wanatumia misamiati ya kilatini na Kifaransa? Na ni kwanini ziwe hizo tuu? Natanguliza shukrani zangu.
 
Mkuu hao walatini au warumi ndio waanzilishi wa mifumo ya kisheria au waendelezaji wazuri waliorasimisha mifumo ya kisheria tunayoiga. Hasa manguli kama akina Marcus Tallius Cicero na wahenga wenzie akina Quintus Hortensius Hortulus.

Mambo mengine hupendeza na kutopoteza maana yake ya asili kama hayajatafsiriwa kutoka lugha ya asili ya muanzilishi kama hao niliowataja japo nao walijifunza hizo study toka kwa utamaduni wa wanafalsafa wa kiyunani(wagiriki).

NOTICE: Haya ni maelezo toka kwa mtu asiyekuwa na taaluma ya sheria bali mpenda historia. Taaluma yangu ni ya sayansi lakini nina hobby ya kusoma historia hivyo naweza kuwa sipo sahihi hata kidogo.
 
Nimekupata mdau,,,
 
Kwa sababu Sheria huazimwa ( sio ya kwao) ukiazima kitu ni lazima ufuate Mashariti, miiko ya hicho kitu!
 
Hii kitu umepata wapi mdau? Nisaidie source ya huko ulikotoa, nimependa maelezo yako.
 
Quick quid plantunt solo solo cedit.
Anything attached to the land form part and parcel of land.
Hahahahahahahahahaha
Usinibip,
Nipe tuu sababu za kuwepo kwa kilatini na Kifaransa kwenye sheria.
 
Anything attached to the land form part and parcel of land.
Hahahahahahahahahaha
Usinibip,
Nipe tuu sababu za kuwepo kwa kilatini na Kifaransa kwenye sheria.
Mkuu, Kilatin hakina mkanganyiko (ambinguities) na kinapunguza wingi wa maneno. LAKINI hiyo inakolezwa na swaga za wanasheria km kawa.
 
Hii kitu umepata wapi mdau? Nisaidie source ya huko ulikotoa, nimependa maelezo yako.
Kwa sasa katafute google habari za Cicero na umaarufu wake kwenye mambo ya sheria na uongozi. Na kazi uandishi.

Kuna kazi zake na mdogo wake zipo tovuti ya serikali ya marekani ni public document nitakutafutia link. Mfano ni How to win Election, n.k.

Naomba nikushauri kasome kitabu kinaitwa IMEPERATA au IMPERIUM na kuna kingine kinaitwa LUSTRUM vyote muandishi ni Robert Harris.
Pia soma hii link
Legal Latin Phrases

Nakumbusha: Maelezo yangu sio ya mwanasheria hivyo naweza kuwa sipo sahihi, niliyochangia ni mtazamo wangu tu na sio matokeo ya utafiti wa mwanazuoni.
 
Habarini wadau.
Kuna lugha nyingi sana duniani, lakini kwanini kwenye sheria utakuta wanatumia misamiati ya kilatini na Kifaransa? Na ni kwanini ziwe hizo tuu? Natanguliza shukrani zangu.
Swali zuri, ukipata muda soma hizi research zitakupa majibu mazuri zaidi na utaridhika

A defense of legal writing by Richard Hyland
Legal language by Peter Tiersman
 
Anything attached to the land form part and parcel of land.
Hahahahahahahahahaha
Usinibip,
Nipe tuu sababu za kuwepo kwa kilatini na Kifaransa kwenye sheria.
Ni zile zile ulizofundishwa kwenye somo la Elimu ya Viumbe (Biology) kwenye Classifications
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…