Kwanini Luhaga Mpina hakuchangia bungeni azimio

Kwanini Luhaga Mpina hakuchangia bungeni azimio

juma30

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
159
Reaction score
459
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina kwanini hakuchangia Azimio la Bunge la Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai? Naomba mwenye kufahamu atusaidie.

4.JPG
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina akiomba dua baada ya kuzuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na mmoja wa waasisi wa Muungano wa Tanzania, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika katika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar, Januari 14, 2022.
 
Tulia alikuwa anatoa muda strategically kulinda heshima ya mwenyekiti, lakini pia wabunge wengi hawakuwepo bungeni siku ile.

CCM wanayo nafasi ya kurekebisha penye mapungufu. Hata kama una nia njema na uko sahihi lakini ni muhimu kuhakikisha unaungwa mkono na watu.

Madaraka yanatoka kwa watu, ukipoteza uungwaji mkono basi yanaweza kunyakuliwa kutoka kwako tena kirahisi kuliko wengi wanavyodhani.
 
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina kwanini hakuchangia Azimio la Bunge la Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai? Naomba mwenye kufahamu atusaidie...
Ule mjadala ulijadiliwa kimkakati, kila kitu kilipangwa.

Hivyo mchango wa Mpina angevurugwa tu na Madam Spika.
 
Waliogopa, wanajua madudu yaliyopo kwenye ule mkataba, hivyo wakajua kama wangempa Mpina hiyo nafasi achangie, angewavua nguo.

Msome kwenye mchango wake wa maandishi ujiuluze kama yupo yeyote kule bungeni ambaye angeweza kumjibu.

Mkataba wa bandari ni wa kihuni umevunja mpaka sheria zetu za ndani, mambo ya aibu sana.
 
Back
Top Bottom