Kwanini Lulu ni mtuhumiwa pekee wa mauaji ya Kanumba?

Kwanini Lulu ni mtuhumiwa pekee wa mauaji ya Kanumba?

Bhaghosha

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
234
Reaction score
183
Wiki iliyopita, Wazee wa Baraza Mahakamani wametoa maoni yao katika kesi dhidi ya msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na kusema mtuhumiwa huyo aliua bila kukusudia.

Ukweli ni kwamba sikufuatilia kujua nini kiliwasilishwa mahakamani lakini mimi kama mtaalamu wa mambo ya usalama wa raia, safety na watoa huduma wa kwanza (First responders) nachelea kusema Lulu kama Lulu na kwa mazingira yaliyokuwepo kwa wakati ule, sioni wapi Lulu anakuwa mtuhumiwa wa kwanza ila tu kama marehemu alikutwa na Sumu mwilini.

Tuangalie 'scenario' zifuatazo:

1. Kama ni kutokana na trauma mazingira yangeangaliwa. Umbo la Lulu na Marehemu vilikuwa tofauti sana. Ile theory ya kusukumwa kwa mazingira ya kiumbo yanamtoa Lulu.

2. Kama kilikuwa ni kipigo, bado mazingira yanamtoa Lulu kwa sababu ya tofauti ya maumbile pia.

3. Lakini kikubwa hasa hapa ni muda toka alipoanguka hadi alipofariki. Hapa ndipo ninapotaka tujadili kwa kina na wanasheria mtusaidie.

a. Je ambulance iliitwa kupitia police? Na ilichukua muda gani? Kama police waliitwa na wakaja baada ya masaa mawili hapo nani wa kulaumiwa?
b. Baada ya kubebwa majeruhi akiwa bado mzima, naambiwa walipitia polisi kuchukua PF 3. Niambie kama nia ilikuwa kuokoa maisha kwa nini wapitie police kuchukua PF3 (kwa uzembe huo Lulu bado anakuwaje mtuhumiwa?)
c. Hapo kwenye PF 3 ilichukua muda gani?
d. Madaktari wanasema (postmortem) ni nini kilimuua Marehemu? Je ilikuwa ni baada ya kuanguka or ni kwa sababu ilichukua muda mrefu kumfikisha hospitalini?
e. Kama ni kucheleweshwa kufika Hospitalini, kwa nini kesi iwaruke woooote hao na kumng’ang’ania aliyesukuma tena ka binti kadogo dhidi ya lnjembe tena bonge?

Wanasheria tusaidieni
 
Back
Top Bottom