Kwanini M-Power haina fixed account option?

geomos

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
625
Reaction score
175
Ninajaribu kufikiri kipi chaweza msaidia mtanzania kujitunzia akiwa, ikikumbukwa kuwa ni jamii ambayo haikuwa na utamaduni huo. Kama unaweza kutoa pesa M-Power kama vile unavyoweza kutoa M-Pesa, siioni ikimsaidia asiye na desturi ya kuweka, maana atazitoa tena akipata dharura au akiwa kwenye starehe. Bora wangeweka option ya kuzifungia pesa zako, mfano kwa mwezi, miezi miwili, mitatu nk. Ili kwa kipindi hicho uweze kuweka lakini huwezi kuzitoa mpaka muda ufike. Ikimsaidia mtu kuona umuhimu wake, na kumfunza kuvumilia ili aongezeke.
 

Umekuja pazuri inaonekana na ww ni mchawi kama mimi, inabidi waanzishe fixed a/c. itasaidia sana kama mimi huwa naweka laki lakini wiki haiish nisha toa tena kwa matumizi ya hooovyo, kama wamo humu watuambie
 
kuna interest zingine za fixed account zinakatisha tamaa afadhali pesa hiyo utolee mahari unaweza ukapata watoto kama faida!
 
kuna interest zingine za fixed account zinakatisha tamaa afadhali pesa hiyo utolee mahari unaweza ukapata watoto kama faida!

Ni sawa lakini, mfano jamaa ameweka laki moja au mbili akailamba hovyoo, si bora hata akiwa amekatwa percent kidogo lakini fedha ataiona, na anaweza akaamua azifunge tena au la, maana hata tunavyotoa M-Pesa tunakatwa pakubwa tu
 
mm kwa ushauri wangu ni bora mtu afanyie pesa biashara yake kuliko kuwapa faida watu wa fixed account!,laki moja inaweza kuwa ndogo kwa mtu asiyekuwa na upeo!,lkn ukichukua hiyo Laki moja ukaenda nayo pale karume ukanunua nguo za kike nzuri kwa 5000,kila moja then unaenda kuwauzia wakina dada ofisini ama vyuoni kwa bei ya 8000 kila moja ukipiga hesabu ni 20 mara 800, hapo kuna faida ya 60000 chapchap,ss ww kaweka pesa fixed account baada ya mwaka na interest ya 15000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…