Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

mkuu madhumuni ya bima ya afya ni tofauti na bima ya mkopo... hii mikopo pamoja na kwamba wanakata bima pia kuna dhamana... mbna stanbic kenya walinirudishia, why hizi bank zetu za ndani hazirudishi?
 
Swali: Kama usingemaliza mkopo, je unafikiri kile kiasi ulichokatwa kama bima kingetosha kulipia mkopo uliobakiza?? Je? Kama hakitoshi fedha nyingine inatoka wapi kulipia deni lako?
ndio maana kuna dhamana mkuu, nadhani unaelewa
 
ndio maana kuna dhamana mkuu, nadhani unaelewa
Ninachofahamu mimi ni kuwa dhamana haitachukuliwa endapo mkopaji kashindwa kurejesha mkopo kutokana na sababu zilizoainishwa labda kifo, ulemavu wa kudumu nk. Hapo ndo bima inachukua nafasi ya kulipia deni. Yaani mfano mtu kafariki, kaweka nyumba kama dhamana, hiyo nyumba haitachukuliwa na kuuzwa na taasisi ya fedha kisa marehemu hakumaliza kulipa mkopo wake.
 
sidhani kama hii itakuwa logic otherwise bank wanatumia kichaka hiki kupiga pesa ndani ya ukopaji kwa kisingizio cha bima ya mikopo
 

shubiri chungu
 
Hiyo elimu ya kirudishwa pesa kwanini hizi benki wasitoe kwa wateja wao. Hao wanakula dhulma tu
 
Vipi unapolipia bima ya gari, na gari isipopata ajali unarudishiwa pesa uliyolipia?!
 
Vipi unapolipia bima ya gari, na gari isipopata ajali unarudishiwa pesa uliyolipia?!
mkuu kuna vitu unachanganya bima ya gari ni tofauti kabisa na hii na hata ulipaji wake, hii bima wanakata bank na makubaliano ni ya maneno hakuna documentation inayoonesha umelipia... mkopo wako ukitoka wao wanakata moja kwa moja kinachoitwa bima ya mkopo kwenye huo mkopo wako, hapa ina maana hii pesa inarudi kwao bank wenyewe na haiendi kwa kampuni wala taasisi za bima
 
Una uhakika kuwa hio hela haiendi kwenye taasisi za bima?
 
Hiyo ni bima sio dhamana mkuu, kwani bima ya gari usipopata ajali unarudishiwa?
 
Hiyo ni bima sio dhamana mkuu, kwani bima ya gari usipopata ajali unarudishiwa?
mkuu kuna utofauti wa bima ya gari na hii,na ndio maana stanbic walinirudishia mkopo wao ulipoisha
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Mkuu acha roho ya kwa nini, hivi uko serious kufananisha bond ya Simu na BIMA? Hivi hiyo 200k ndio Iwe bond ya 10m ulizovuta? Hivi uonagi wenzako bond zao huweka nyumba na Mali nyingine zenye thamani zaidi ya kile walichopewa?

Tatizo kubwa watu hatupendi kusoma maandishi mengi, BIMA ni moja ya sharti la kupewa kwako mkopo, na ungesoma kabla ungeelewa vizuri ila kwa sababu ulikuwa na hamu ya manoti muda huo hukujali. Nadhani ndio maana wenzako hawakujibu simply they know your fault.
 
Akili yako kama yangu mkuu, umekata bima ya gari baada ya miaka 5 unaliuza kwa mtu mwingine ana unaachana na mambo ya magari au chombo chochote cha moto, vp hapo mleta mada unataka bima wakulipe hela yako hiyo.?
 
mkuu roho ipi ya kwa nini? hiyo 200K sio ndogo ingekuwa ndogo wasingechukua..., stanbic bank branch ya kenya wao mbona walinirudishia mkuu...na kumbuka hao wanaoweka bond nyumba lakini pia wanakatwa hii bima kwenye mikopo wanayochukua sasa why wasirudishiwe pesa yao wanapomaliza deni lao
 
Akili yako kama yangu mkuu, umekata bima ya gari baada ya miaka 5 unaliuza kwa mtu mwingine ana unaachana na mambo ya magari au chombo chochote cha moto, vp hapo mleta mada unataka bima wakulipe hela yako hiyo.?
wabongo tunapigwa sana maana hatutaki kufuatilia vitu, hawa wajinga wanatupiga sana pesa kwa sisi kutotaka kujua vitu
 
Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.

Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.

Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.
 
sasa hawa si ra di bi hawakunipa na sidhani kama wanawapa wateja wao hii cover note, wao wanakata juu kwa juu tu unapewa maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…