Kwanini madalali wameyashikilia masoko na kusababisha bidhaa kutoshuka bei?

Kwanini madalali wameyashikilia masoko na kusababisha bidhaa kutoshuka bei?

yogan

Senior Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
133
Reaction score
91
Mimi ninauza genge la mboga mboga na matunda.Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa biashara katika masoko ya jijini Dar es salaam kama Mabibo, Buguruni, Temeke, Stereo na Ilala.

Katika masoko yote haya hakuna mkulima anaruhusiwa kuuza BIDHAA zake sokoni. Mzigo unapofika sokoni Wanakabidhiwa MADALALI ndo wanauza kadiri ya makubaliano na mkulima.

Chakusikitisha ni kwamba hawa jamaa wanafaidika sana hata kuliko wakulima wa nchi hii kwani wanatumia faida ya wakulima kutohusika kuuza BIDHAA nao kupandisha bei za BIDHAA kiholela.

imefikia hatua hata BIDHAA zikiwa zimefurika sokoni bado wanaziuza bei ya juu Jambo linalosababisha wakulima kupata hasara kwani kuna bidhaa huharibika kwa kukosa wateja. Mpaka sasa Mimi sioni umuhimu wa madalali sokoni kwani wanaleta maisha magumu bila sababu za msingi.

Hawa jamaa wakuondolewa bidhaa zitauzwa Kwa mfumo huru WA kibiashara na kuzingatia chain ya demand na supply ambayo inaweza kutupa unafuu wa maisha yetu.
 
Hiyo kukabidhi mzigo kwa dalali ni utaratibu rasmi?

Endapo ukigoma kukabidhi mzigo kwa dalali ili uuze mwenyewe, ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mkaidi?
 
Inaumiza sana.halafu unasikia wapuuzi wanasifu serikali.
 
Wa kusaidia hilo ni Serikali tu,kama kalala usingizi unategemea nini?
Tuwaamshe Kwa kweli hili Jambo linamfanya mkulima anakuwa Masikini kila siku. MADALALI hawana uchungu na mali za mkulima hata kidogo ona hapo ndizi zimeoza wamegoma kushusha bei basi wangetoa hata sadaka Tu lkn MADALALI wamekomaa sana
IMG_20240415_095312.jpg
 
Hiyo kukabidhi mzigo kwa dalali ni utaratibu rasmi?

Endapo ukigoma kukabidhi mzigo kwa dalali ili uuze mwenyewe, ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mkaidi?
Huu ni utaratibu unaoratibiwa na masoko niliyoyataja
 
Waumini wakubwa wa uchawi nchini;
1. Wabunge
2. Madalali/Mission town
3. Wanawake
4. Wafanyabiashara
5. Watumishi wa umma

Ukitaka kupambana na madalali, pambana na uchawi!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wa kusaidia hilo ni Serikali tu,kama kalala usingizi unategemea nini?
Serikali hakuna kitu wanaweza fanya cha zaidi wataharibu flow ya biashara. Dawa yao hawa ni kuwaondoa katika mnyororo wa biashara na thamani kwa kutumia mbinu za kisasa za kibiashara.

Dawa yao inachemka.
 
Hiyo kukabidhi mzigo kwa dalali ni utaratibu rasmi?

Endapo ukigoma kukabidhi mzigo kwa dalali ili uuze mwenyewe, ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mkaidi?
Tatizo huwezi lima na kuuza mwenyewe inagharimu muda na fedha, utapata hasara.
 
Serikali hakuna kitu wanaweza fanya cha zaidi wataharibu flow ya biashara. Dawa yao hawa ni kuwaondoa katika mnyororo wa biashara na thamani kwa kutumia mbinu za kisasa za kibiashara.

Dawa yao inachemka.
Tukifanikiwa hawa bidhaa nyingi za masokoni zitashuka bei na mtaona maumivu ya ughali WA maisha unapungua
 
Tukifanikiwa hawa bidhaa nyingi za masokoni zitashuka bei na mtaona maumivu ya ughali WA maisha unapungua
Na kikubwa zaidi mkulima atapata zaidi ya anavyopata sasa wananyonywa Sana
 
Mimi ninauza genge la mboga mboga na matunda.Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa biashara katika masoko ya jijini Dar es salaam kama Mabibo, Buguruni, Temeke, Stereo na Ilala.

Katika masoko yote haya hakuna mkulima anaruhusiwa kuuza BIDHAA zake
 
Madalali ni watu wabaya kabisa dalali hana tofauti na mwizi, kwann serikali isiingilie kati hili jambo, make kila mzembe, kila mwenye tamaa ya pesa bila kuvuja jasho na kutapeli apa dar anakimbilia kua dalali..
 
Tatizo wakulima wengi teknolojia imewapita kushoto,huu ni wakati wa kubadilika na kutangaza bidhaa zako mitandaoni
 
Back
Top Bottom