Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Wakuu hali imekuwa tofauti kabisa na matarajio ya wengi. Madikteta kutoka nchi nyingi ikiwemo Tanzania hawajafurahishwa na ushindi wa D Trump.
Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza uliomalizika 2021 Trump alikosolewa kwa kuwanyoosha viongozi madikteta ikiwemo serikali ya Magufuli kwa kunyimwa fedha za miradi za MCC, viongozi wake wahuni kama makonda wakilimwa ban ya kuingia States.
Huko Asia nako Irani walikipata kwa raia wake kutoruhusiwa kuingia Marekani na mbinyo wa Vikwazo kuimarishwa zaidi.
China kwa upande mwingine ilikipata Cha mtema Kuni kwa kampuni zake kuwekewa vikwazo vya kibiashara na Marekani wakati wa utawala wa Trump. Trump amerudi na hii haijawafurahisha wahafidhina wa kiafrika pamoja na makundi yote ya kigaidi.
Je, kurudi kwa Trump kunaweza kuleta adhari zipi kwa Afrika, Asia na Ulaya kwa viongozi wahuni?