Kwanini magazeti ya Serikali na CCM hayaripoti kesi ya Mbowe?

..nakumbuka kesi ya UHAINI ya miaka ya 80 ilikuwa inaripotiwa ktk magazeti yote.

..sielewi kwanini kesi kubwa ya UGAIDI inayomhusisha mwenyekiti wa chama cha siasa na waliopata kuwa askari wa Jwtz hairipotiwi ktk magazeti ya serikali, na ya Ccm.
 
Kwani yakiripoti ndio mwenendo wa kesi utabadilika?

Hii ni kesi nzito kwenu chadema sababu inamhusu Bosi wenu mkuu.
Lakini haiwahusu watanzania wengine.
Kumbuka sio kila mtanzania ameweka siasa mbele.
Pia kumbuka kwamba kila mtu anao ufuasi na itikadi yake tofauti.

Usilazimishe jambo lenu liwe la kila mtanzania.

Wewe kashindie mahakamani na wenzio watashindia kwenye kahawa na wenye majukumu yao wataelekea kwenye utafutaji wa riziki za familia zao.
 
Utoto unakusumbua. Ugaidi ni jambo kubwa sana katika taifa lolote, hivyo hata namna inavyo ripotiwa kesi hiyo lazima iwe kwa uzito mkubwa sana tofauti na hizo kesi zenu za kubaka kuku.
JokaKuu hapo juu amekumbusha kesi za zamani zilivyokuwa zina ripotiwa, unadhani ni sahihi kwa sasa kutoripoti hicho wanacho Dhani ni ugaidi kama sio kuwa ni aibu kwa yanayotokea?
 
Akifungwa wataripoti
Mashahidi wako 24 na 10 tayari wakiwemo Principle key witness 5 tayari wametoa ushahidi na hakuna aliyeonyesha beyond reasonable doubt hata viashiria vya ugaidi, hapo wanamfungaje?
Tambua kesi hii inafuatiliwa hadi huko EU na UN
 
Itakuwa dhamiri inawasuta. Ni sawa na kwenda kulia kweye msiba wa marehemu ambaye ulimuua mwenyewe.
 
Tafakari
 
Yaaani umekamata magaidi ukatangazia dunia lakini unaogopa kuinyesha ushahidi wa kiwaumbua hao magaido
Kila wakibanwa wanakuja na hoja 'siwezi kusema kwa sababu za kiusalama'. Uhuni mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…