Kwanini Magoli anayokosa Bocco kufunga wengine hawakosi?

Kwanini Magoli anayokosa Bocco kufunga wengine hawakosi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
John Bocco ni Mchezaji wa Simba anayelaumiwa sana na mashabiki mbalimbali wa Simba na nje ya simba kwa kukosa magoli akiwa uwanjani.

Lakini siku Bocco asipocheza huwa hatuoni wachezaji wengine wa Simba wakikosa magoli ambayo Bocco hukosa.

Huwa sielewi ni kwa nini wachezaji wengine wa Simba hawakosi magoli mengi kama akosavyo Bocco.

Kwani yale magoli anayokosa Bocco huwa yanatoka wapi ambako wachezaji wengine wa simba wanashindwa kuyapata?
 
Mshambuliaji anaejua kuji position mnapokua na mpira ni rahisi kupata pasi za mwisho za kufunga.

Ao unaosema awapati iyo mipira mingi ya kukosa magoli kama anayopata Boco ni mapungufu ya mchezaji binafsi.
 
Kwa maana nyingine wachezaji wengi wa Simba hawana uwezo wa kukaa kwenye nafasi za kufunga kama John Bocco!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi wewe ni utopolo aka kidimbwi.

Sijawahi kusikia hizo lawama kwa wapenzi wa Simba.Wala hakuna anayemlaumu Boko.

Kwa taarifa yako tumemisi uwanjani na tunajua alikuwa injury.

Acha fitna zako za kishamba na ni dalili ya uchawi kutaka kujaribu kuua morali ya wachezaji wetu.

Vinginevyo jitahidi kuujua mpira kwa kuangalia mechi za walioendelea kwenye soka kwa mfano ligi za ulaya.
 
Back
Top Bottom