Kwanini maisha yamekuwa kazi tu, kazi! Mbona hatuna muda wa raha?

Kazi kazini mimi naamka 11 narudi 12 au saa moja sikuzote za week..
kwelii kuna muda nawaza mbona ni kama nateseka ?
Nakuelewa sana! Wakati mwingine tunapokazana sana kazini, tunajikuta tunateseka kimawazo. Hata hivyo, tunapaswa kutafuta njia za kupumzika na ku-refresh akili, japo kwa muda mfupi, ili tuendelee mbele kwa nguvu zaidi.
 
Kupumzika Hadi kaburini ndugu yangu
 
Kupumzika Hadi kaburini ndugu yangu
😀😀, umenichekesha! Inaonekana sasa ndio msemo maarufu – 'kupumzika hadi kaburini.' Lakini unajua, ingawa ni kweli hatuna muda mwingi wa kupumzika kwa sasa, bado ni muhimu kujaribu kutenga muda wa kupumzika kidogo ili tusiishi maisha ya presha pekee. Hata mapumziko mafupi yanaweza kuleta tofauti kubwa kwa afya zetu na furaha.
 
Hapo ndipo tunapokumbushwa kuwa ajira nayo ni baraka. Ingawa tunalalamika kuhusu jinsi kazi zinavyotufanya tushindwe kupata muda wa kufurahia, bado kuwa na kazi ni jambo la kumshukuru Mungu. Ni suala la kutafuta ile ‘balance’ tu.
Kikubwa ni kutafuta balance. Binafsi nayajua maisha ya ajira rasmi,maisha ya ajira isiyo rasmi (wengi wanaita kupambana) na maisha yasio na ajira (upo-upo). Ndugu kama una uhakika wa mahali pa kuamkia kesho yako,na mwisho wa siku kuna kitu kinaingia mfukoni,kinakuruhusu kupanga mipango ya hata kesho yako tu,shukuru sana huku ukitafuta balance.
 
Umenena vyema tutaangalia🤝🙏🙏
 
Kabisa mkuu..hilo ndio la muhimu kwenye haya maisha
 
Bora kwenda mbinguni, maana huko nasikiaga hakuna kufanya kazi, hakuna njaa, ni kuimba mapambio na kufurahi...!
Kabla hujafika huko mbinguni, hapa katikati napo upumzike. What if usifike hata huko mbinguni kama tunavyoambiwa
 
Mfumo wa maisha ya kibepari umetufanya binadamu tuwe kama mazombi!

Binadamu tumegeuka kuwa kama mashine ambazo kazi yetu ni kutumika to the maximum ili kuzalisha na kutengeneza faida, bila muda wa kupumzika na kuishi. Na hii haijalishi kama umeajiriwa au umejiajiri wote mchakamchaka ni ule ule. Kila mtu yuko busy kukimbizana kukusanya hela ili awe na "vitu vizuri", tukidhani kwamba kuwa na vitu vizuri/vya gharama kubwa ndio maisha mazuri.

Ukija kuangalia ni kipi hasa cha maana tunachopambania unakuta ni hakuna. Tunakimbizana kutwa kucha kutafuta vitu "material" ambavyo mwisho wa siku wala havitupi furaha, na wala sio muhimu kiivyo kwa maisha yetu. Na kila siku vinatoka vitu vipya ambavyo inabidi tuzidi kupambana zaidi ili tuwe navyo kwa kuaminishwa kwamba bila kuwa na vitu "latest" hatuwezi kuishi kwa furaha..!
 
Mada nzuri sana shukrani 🤝

Me nawaza utajiri namba moja ni rasilimali watu, kupambana mwenyew ngumu sana lazma kuwatumia waliokuzunguka, usipojituma utatumwa! Social circles muhimu sana iwe kikundi cha mikopo ya halmashauri, upatu kina mama, cha kufanya mazoezi fitness, cha kidini whatever u have to belong somewhere na hilo ndo linanitesa coz ni mgumu kufungamana na watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…