Kwanini maiti hazitolewi kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti baada ya saa 12 jioni?

Kwanini maiti hazitolewi kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti baada ya saa 12 jioni?

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,659
Habari kwenu wanabodi, naleta swali hili kwenu,

Je, ni kifungu gani cha sheria kinacho regulate utoaji wa maiti kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti maarufu kama mochwari (mortuary)? Maana katika nchi yetu hairuhusiwi kutoa maiti baada ya saa 12 jioni. Sasa nikaona nililete swali hili huku kwa kuwa ni swalili intelligent!

Majibu yenu itapendeza zaidi nikipewa sheria na kifungu kinacho regulate utaratibu huo. Lengo ni kuelimishana ili kupata uhalisia na kuacha kufanya kazi au kuishii kwa mazoea.

Asanteni.
 
Swali zuri watu hospitali nafikiri mna ufahamu na hili na lawyers mtusaidie
 
Habari kwenu wanabodi, naleta swali hili kwenu,

Je, ni kifungu gani cha sheria kinacho regulate utoaji wa maiti kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti maarufu kama mochwari (mortuary)? Maana katika nchi yetu hairuhusiwi kutoa maiti baada ya saa 12 jioni. Sasa nikaona nililete swali hili huku kwa kuwa ni swalili intelligent!

Majibu yenu itapendeza zaidi nikipewa sheria na kifungu kinacho regulate utaratibu huo. Lengo ni kuelimishana ili kupata uhalisia na kuacha kufanya kazi au kuishii kwa mazoea.

Asanteni.
Hata usiku zinatolewa tu, ni pesa yako mkuu.
 
Sio kweli, ni mipango tu , mm nimewahi kuhuhudia maiti inatolewa saa 1 jioni!
 
Nakumbuka nilifiwa na mtoto wakati nashughulikia masuala masuala ikatinga saa 12 kwenda kuchukua mwili wakaanza kugoma goma basi nikatumia tu ushawishi fulani nikapewa na ndipo hapo na mimi nikajua kumbe kuna muda ukifika hupewi mwili.
 
Mkuu again ,issue hii ilitakiwa isilete usumbufu kwa yeyote yule, why nchi haina private undertakers?,ilitakiwa kila mfiwa kupeleka mwili wa mpendwa wake kwa undertaker anayemtaka ,na muda wa kwenda kuchukua mwili inakuwa ni makubaliano yenu, sasa serikali imehodhi hadi maiti, rushwa,rushwa, rushwa kwa kwenda mbele, mwananyamala mortuary inanuka rushwa
 
Back
Top Bottom