Kwanini majanga ya moto hutokea Jumapili mara nyingi?

Kwanini majanga ya moto hutokea Jumapili mara nyingi?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Waungwana Tanzania tunapigwa kizembe sana . Hasa hii serikali ya BITOZO wahuni wanafanya lolote wanalotaka.

Inakuwaje ajali za moto zitokee kuamkia Jumapili tu ni coincidence ya namna gani hii..

Aisee kuna watu wanapiga sana hela kupitia haya majanga ya moto halafu hawana wa kuwawajibisha wala kuwafanya lolote.

Leo moto wa Tanga wameangalia watu tutakuwa tumeconcetrate na game ya Simba na Yanga wakafanya yao wakijua Kelele hamna.

Aisee nchi ngumu sana, hii huko Ghalani watu watakuwa wamefanya madudu hatari.

RIP JPM.
 
Du mkuu hujui kuna ghala la TRA limeungua huko
Me nilikua barabarani siku nzima kutoka point A kwenda point B so sijasikiliza wala kusoma chochote kuhusu Tanga, hapa ndo nashtuka kuskia haya.. Sasa hilo ghala la TRA ni ghala la document au?
 
Nimesikia redioni asubuhi hii, ghala la TRA lililopo katika bandari ya Tanga ambalo huhifadhi bidhaa mbalimbali za wafanyabiashara walioshindwa kuvikomboa limeteketea lote.
Vitu kama pikipiki, baiskeli, nguo na vitu vingine mbalimbali vimeteketea.
Miaka ya nyuma kulikuwa na kawaida ya kupiga mnada bidhaa mbalimbali ambazo zilishindikana kukombolewa.
 
Nahisi vilivyokuwa ndani ya ghala vitakuwa vilishatolewa kitambo kabla ya moto kuzuka. Moto umetumika kupoteza ushahidi.
 
Back
Top Bottom