Kwanini makampuni makubwa Duniani wanawekeza nchini Kenya?

hayaland

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
712
Reaction score
399
Nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini makampuni makubwa kama ya magari mfano NİSSANİ,VOLVO,SCANIA na mengine ikiwa ni pamoja na mashirika makubwa ya ndege kama vile BRITISH AIRWAYS,AMERICAN AIRLINES,EMIRATES,ITALIAN AIRWAYS,KLM,na mashirika mengine ya ndege yana safari zake nchini Kenya,

Vyombo vya habari vikubwa navyo haviko nyuma katika kuwekeza nchini Kenya,CNN,SKY,BBC,AL JAZEERA na vingine vingi wanazo ofisi zao Nairobi,ndo maana hata habari ndogo ndogo za Kenya zinarushwa na vyombo hivyo.
Tanzania tunao mkakati gani kuwashawishi wenye makampuni makubwa kama haya japo sio yote kuja na kuwekeza nchini mwetu? Nimeona hata kama takwimu zinadai uchumi wetu unakua kuliko wa Kenya bado hatutaweza kushindana na wenzetu Kenya.
Hata mabarozi wanaoziwakilisha nchi zao,kama barozi anawakilisha nchi yake katikaTanzania na Kenya,barozi huyo atapenda zaidi kuishi Kenya na sio Tanzania,hapa nchini atakuja tu na kurudi Kenya .
Pamoja na história kutuhukumu kuwa Kenya wawekezaji walikuja miaka mingi enzi za ukoloni(colonialism) bado nchini yetu inalo la kufanya ili KUWEZA kuwa na wawekezaji wakubwa kutoka ulaya na Marekani.
 
Wanaiogopa ccm kama pogaba anavyomuogopa Lissu
 


Kwa sababu Kenya ina uchumi mkubwa AM na pia purchasing power ya Kenya ni kubwa klk zote AM isitoshe walibahatika akina Zito Kabwe, Tundu Lisu, Lema & Co. hawakuzaliwa huko vinginevyo hayo Makampuni yote yangesepa!
 
ICRC pia ipo Nairobi

Reasons;

1st point:

-Language barrier..[English language-the International Lingua franca] to which most of we Tanzanians are not accustomed and in which, even those few who may hardly fumble to speak it, are not fluent any way.


2nd point:

-Economic system of this country; that, Tanzania was fundamentally based on the dictates of socialism and self reliance. This pragmatic realities, ipso facto, did, I think, put off the western capitalist nations from popping into it for investment or so.

-Etc
 
Kabla Kampuni haijafanya uwekezaji inafanya analysis nyingi.Inaangalia Gharama za kuendesha biashara katika nchi husika.Inaangalia Labour force katika nchi husika.Aidha Kampuni inafanay tathmini ya ulinganifu wa Soko la bidhaa itakapokuwa imezalisha.Sisi Tz gari mpya nyingi hununuliwa na Serikali (Kuu,za mitaa na mshirika ya umma),International NGOS,Private companies za Kigeni na Kidogo watu wa Dini.Wananchi wengi hununua used/mitumba.Kwenye magari unahitaji angalau soko la gari mpya laki 1 kwa mwaka.Hapa TZ middle class ni ndogo ukilingamisha na Kenya.Nimefanya kazi na Wakenya na mara kadhaa kutembelea nchi za EAC na SADEC na hivyo kuna utofauti wa nchi ingawa tu majirani.Miundombinu pia ni factor.Wakati sisi tunapiga sound ya reli ya Standard Gauge,wenzetu tayari treni zinatembea.Tunapiga sound za Fly over wenzetu wana vipande kadhaa pale Thika Road na kwingineko.Heshima aliya nayo mkenya kwenye Kazi siyo sawa na Mtz...
 
Mkakati mmoja wapo ni kupanua viwanja vya ndege ili mashirika makubwa ya ndege yaje kuwekeza,Pili ni kusimika mitambo ya rada ya kisasa ya kuongozea ndege ili ziruke kwa uhakika bila kuleta ajali sambamba na ulinzi wa anga la tanzania kwenye hili Kenya walitutangulia,tatu kuhakikisha njia za usafirishaji haraka wa maligafi za viwandani na bidhaa zake hapa tumejaribu ujenzi wa reli za Umeme toja dar kwenda mkoani,Kumbuka miradi ya Umeme inayoendelea kujengwa itasaidia upatikanaji wa nishati viwandani,ngoja vyote vikikamilika tuone kama hawatakuja kuwekeza Tanzania
 
Hili swala nila kihistoria zaidi. Kenya wamekuwa karibu na Western hasa UK toka wapate uhuru. Ukiangalia hata Queen Elizabeth baba yake King George VI alipokufa, Elizabeth alikuwa yupo Kenya. Pia Kenya ni kati ya nchi za Africa zenye British passport holders wengi.
Na Kubwa zaidi ni wapo close to western cultures such as language na pia watambulika kuwa ni wasomi zaidi.
 
Kweli kabisaaaa
 
Iyo ni propaganda ya Kenya tu, baada ya kuona ukuta wa mererani kuzinduliwa ,vita ya kiuchumi ni ngumu sana na inaitaji umakini wa khali ya juu, Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki na kimlinda Raisi wetu JP Magufuli
 
Watanzania wakiongozwa na wanasiasa was upinzani wanataka maendeleo ila hawataki process inayoleta maendeleo. Ukijenga miundombinu Kama reli, ndege, Barabara, umeme nk wanapinga kwa nguvu zote. Ndo hawa Hawa wanobeza uwekezaji wa SGR, ufufuaji wa atcl nk.. then wanakuja kuuliza maswali Kama haya ya mleta mada

Watz hawajui wanataka Nini au wanataka maendeleo ila hawapendi the process yakufikia maendeleo
 
Duniani Kenya ipo Nafasi ya 80 kwa uwekezaji na Tz ipo 137.
 
Kwa sababu Kenya ina uchumi mkubwa AM na pia purchasing power ya Kenya ni kubwa klk zote AM isitoshe walibahatika akina Zito Kabwe, Tundu Lisu, Lema & Co. hawakuzaliwa huko vinginevyo hayo Makampuni yote yangesepa!
Hivi kumbe hao wakina lema ndo walimfanyia umafia dangote???nyumbu wa kijani bhn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…