Ni kazi ya kamusi hasa. Hiyo kwamba utayatumia ama la ni juu ya watumiaji.
Miongoni mwa sifa muhimu ya lugha ni kukua, basi kila yanapokuja maneno mapya na kukubaliwa kimatumizi ktk jamii huwekwa rasmi pia katika KAMUSI.
Kamusi za Lugha ya Kiingereza zina baadhi ya maneno mengine yameandikwa katika mabano; (
ancient, formal) ~a zamani, rasmi, n.k. hudhirisha namna wingi na mbadala wa maneno ulivyo ktk lugha. Sasa neno sehmu za siri wengine huita utupu, lakini jina rasmi ni uchi. Ila uungwana tu sawa na mahali ndio unaopelekea mtu kuweka tafsida nyiiiiiingi.
Pia tusi ni:
Tusi ni matumizi mabaya ya kauli au neno. Neno laweza kuwa tusi kwa mtu A na lisiwe tusi kwa mtu B kutegemeana na muktadha wa mazungumzo. Mimi ni mweusi lakini kuna mazingira ya kuzungumzia weusi wangu kutafanya lionekane ni tusi ama la!.
Sasa binadamu ukimuita k**a, mbwa, kima, moja kwa moja umemtukana.
Lakini binadamu mwenye sifa stahiki ya ushoga, usenge, upumbavu, n.k. ukimuita hivyo si tusi, Linakuwa TUSI kwa LISIYEMUHUSU k.m. rijali, kidume, mwerevu n.k.
Huo ndio muono wangu