Kwanini maovu watende CCM, lakini walaumiwe CHADEMA?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kila wakati huwa sielewi akili za watu wanaowalaumu CHADEMA kwa matendo maovu yanayotendwa na CCM.

Serikali kwa sasa inaongozwa na CCM (hakuna Serikali ya CCM) kwa ivo kila baya linatendwa dhidi ya CHADEMA na Serikali, ni lazima liwe linatokana na maagizo ya CCM.

Kwa mfano John Magufuli akiwa Rais wa Tanzania, kinyume kabisa na Sheria zote za nchi, alizuia mikutano ya vyama vya siasa isipokuwa ile ya CCM.

Lakini CHADEMA ikawa inalaumiwa ni kwa nini inalazimisha kufanya mikutano au ni kwa nini hailazimishi kufanya mikutano.

Misaada ya nchi za nje inayotolewa Kwa Tanzania inatolewa wakati CCM ikiwa madarakani. Lakini CHADEMA ndiyo inayolaumiwa kuwa ikiingia madarakani misaada itatolewa Kwa masharti ya kukubali ushoga.

Lakini CCM wenyewe ndiyo waliomkana Makonda kuwa staili yake ya kupambana na mashoga si msimamo wa Serikali. Sasa hapo CHADEMA inahusikaje?

Watanzania wanataka Katiba Mpya, CCM hawataki. Badala ya kuwaeleza watanzania ni kwa nini wao CCM hawataki Katiba Mpya, wanasema CHADEMA hawana shukrani kwa kutaka Katiba Mpya.

CCM Kila wakati yenyewe ndiyo hutenda uovu lakini Mwisho wa siku huwasakama CHADEMA.
 
Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma na kufuatilia mambo ya msingi. Ccm knows this so whatever information mbaya wanayo izusha kwa chadema ni rahisi mno wao kuamini, hata kama chadema wataonyesha ukweli
 
Kabisa... Wamevunja Katiba Yao, lakini wapo bize kusema "Lissu hawezi kutoboa"

Sasa kuvunjwa kwa Katiba ya CCM kunahusiana vipi na kutotoboa Kwa Lissu?
 
Back
Top Bottom