Uchaguzi 2020 Kwanini Marekani, Umoja wa Ulaya wanamuunga mkono Tundu Lissu? Kosa la Magufuli ni lipi?

yani unafikiria swali alafu unajijibu mwenyewe ,kweli sisiemu mmepagawa
 
USA mbona wamesema wazi kuwa wako neutral na hawaungi mgombea yoyote mkono!Ila wameongeza wataangalia kwa karibu mchakato wa kampeni,kupiga kura na baada ya kupiga kura na kama kuna uminywaji wa haki basi watachukua hatua accordingly!
 


Mkuu GUSSIE natumaini umekunywa chai vizuri.
Tukubali tukatae Mabeberu wametushika pabaya,hii ni kwasababu Serekali ilikuwa ikifanyakazi kwa nguvu badala ya kutumia akili.

Chukulia mfano suala la Korosho,nguvu ilitumika badala ya akili na maarifa.
 
Kwa sababu: ndio Rais wa awamu ya6
#NIYEYE Rais Lissu ✌🏽✌🏽✌🏽✌🏽

Kwa sabababu: Lissu najua kidhungu na mpigania haki zetu Watanganyika, wataongea watasikizana na wataelewana.

Kwa sababu: Mtupoli hajuhi kidhungu, anajua kuua tu, sasa wa nini.?
Wataongea nini, mauaji ya Watanganyika.?
 
Kufikiria ni haki yako sheikh.
 
Mirija yao ya ulaji imekatwa, Wanataka huyo kibaraka wao airejeshe. Thubutu, watanzania tupo imara. Mkoloni out, beberu out, Lissu out.
 
Uwanja upi haupo sawa mkuu

Kwani lissu hajaruhusiwa kufanya siasa

Mbona si lipumba au Membe?
Hapo ndo tunqpoona ufinyu wa fikra zako. Hivi CCM wahangaike na Lipumba kwa lipi hasa? Timu inapambana na mshindani haipambani na Mshiriki. Unadhani Marekani kuna wagombea Urais wawili tu hadi Trump ahangaike na matokeo ya shule ya Joe Bidden peke yake?
 
JAICA na wazungu wapinawapi naona kamavile umechanganyikiwa!
 
Ili kunigesha ngoma waambieni waje wapige kura ili wamsaidie kuwa rais wetu
 
Hahahahaha si mlijiandaa kuharibu uchaguzi eeeh??? Sasa kaeni Mkao wa kula.

Tundu Antiphas Lissu ndo Raisi wako wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 

Tulikuwa tunasema nchi hii sio mali ya Magufuli mlikuwa hamuelewi. Uonevu na ukatili wote dhidi ya wapinzani upo wazi, na ushahidi tunao. Hata ww ukiwa baba wa familia huwezi kuwalawiti na kuwaua, jamii ikakaa kimya kisa eti unaleta chakula na kuwasomesha. Chaguzi za nchi hii toka Magufuli kaingia madarakani zote zimenajisiwa, huku tukishuhudia ukatili, ushenzi, unyama na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi. Haya yote yamefanyika kwa maagizo ya rais, chini ya uratibu wa jeshi la polisi na tume isiyo huru ya uchaguzi. Kwanini wazungu wasiingilie wakati taasisi za kutoa haki ziko upande wa ibilisi?

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani kulikuwa na uhuru wa kufanya siasa, uhuru wa habari, tulikuwa tunaona midahalo na mijadala huru kwenye media mbalimbali kujadili mustakabali wa nchi. Sasa hivi hakuna mambo hayo, bali wote tunatakiwa tumsujidie Magufuli. Dunia haiwezi kufumbia macho tabia hizo. Sasa hivi rais anapita anatishia wananchi kuwa akichaguliwa hatapeleka maendeleo sehemu ambayo hajachaguliwa mwanaccm, huku tume na jeshi la polisi likiwa kimya kabisa. Mbona hao wazungu huwa wanatupa misaada kwani wamepewa kura na nani? Tumesema tume hii ya uchaguzi inatii matakwa ya Magufuli, hivyo hatuna imani nayo. Tuna imani tu na uchaguzi huu iwapo wamerakani ndio watausimamia maana tume hii tayari ina matokeo mfukoni. Ni vyema Marekani wakasogeza manuwari ya kivita hapo bandarini kuepuka wananchi wasioikubali ccm kuhujumiwa ushindi wao kwenye uchaguzi huu.
 
Kudhulumu haki ya watu ya kuishi, kiburi, jeuri, dharau, udicteta, ufisadi, uongo, ubaguzi wa kisiasa na kiukabila, uvunjifu wa sheria na katiba, hayo ni robo tu ya mengi yanayomuhusu alcohol.
 
Kusema kuwa demokrasia ipo chini haimaanishi wanamuunga mkono Lissu na kumkataa Dr. Wanachomaanisha ni kuwa pawe na uwanja sawa wa kuombea kura, na wananchi wenyewe wachague wanayemtaka.
Kilochowashtua zaidi ni ule uchaguzi Wa serikali za mitaa uliopita ndo mana wamekuwa na wasiwasi na uchaguzi huu ccm wanaweza Fanya tena uharamia Wa kijinga kama huo walioufanya.
 
Uwanja upi haupo sawa mkuu

Kwani lissu hajaruhusiwa kufanya siasa

Mbona si lipumba au Membe?

Lipumba na Membe sio wapinzani, bali ni backup za ccm kupitia upinzani.
 
Kusema kuwa demokrasia ipo chini haimaanishi wanamuunga mkono Lissu na kumkataa Dr. Wanachomaanisha ni kuwa pawe na uwanja sawa wa kuombea kura, na wananchi wenyewe wachague wanayemtaka.
Kwa nini washike mabango? Mwenye akili timamu hawezi kushabikia lolote kutoka nje na hawawezi kutuchagulia Rais Kwa vitisho vyao tutampa tumtakaye, si wote tumeshikiwa akili, wanakuja na kisingizio cha demokrasia, hawakuiona miaka yote waje, waione kwa Lisu,
 
Hii ina maana mabeberu wamewakamata hadi wananchi ili wamumuunge mkono Lissu?
Usiwadharau watu namna kwa hilo neno la kijinga Ubeberu


Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwasababu magufuli aliwakazia kwenye mikataba ya madini na rasilimali za nchi yetu.sasa wanamuunga mkono Lissu kwakuwa atawagawia rasilimali zetu watakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…