Uchaguzi 2020 Kwanini Marekani, Umoja wa Ulaya wanamuunga mkono Tundu Lissu? Kosa la Magufuli ni lipi?

Kuna mtu kamwelewa huyu mwanamizengo au ni mimi tu sijamuelewa
 
Katika chaguzi zote Marekani na nchi zote duniani ambazo zinaamini katika demokrasia ya utawala wa sheria, hata humu Afrika. Wamekuwa na kawaida ya kutoa matumaini yao katika chaguzi mkuu wa Rais, wabunhe na madiwani, kwamba wanafurahia na kupongeza demokrasi lakini wanasisitiza umuhimu wa uchaguzi huru pasipo kuwa na vurugu. Kwa maana historia inaonesha nchi nyingi na hasa Afrika zilibadili siasa za nchi zake na kuingia kwenye siasa ya vurugu katika kipindi cha kampeni na kuelekea uchaguzi.

Hao hawanaga upande wa Chama cho chote cha siasa, upande wao hao ni demokrasia basi. Sisi tuwe na imani ya ushindi kwa CCM baada ya uchaguzi na kwa sasa tueendelee na kukusanya kura nyingi za ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi mkuu 28 Oktoba, 2020.
 
Hakuna sehemu wametaka kuwachagulia rais. Wanaochagua rais ni wananchi, mimi, wewe na yule. Wanachotaka ni fair play kwa wote. Kumbuka kuwa yakitokea ndivyo sivyo e.g. vita, wao ndo hubeba mzigo mkubwa ( kuhudumia wakimbizi, kutoa misaada ya kibinadamu, etc ). Wanachukua kinga kabla ya hatari
 
Hao unaowaita mabeberu, mara wafadhiri wa maendeleo mara nchi wahisani wanaitambua nchi yetu vizuri mno zaidi yako wewe. Kwa kuwa kupitia tu ktk sayansi na teknolojia wanautambua ufedhuli na udhalimu wote wa serikali ya awamu hii.

Unafikiria hawana ushahidi juu ya mauaji ya MKIRU, upoteaji wa watu wenye kukinzana na watawala, watu kuumizwa, kuuwawa na hata kuwa "intimidated" ktk kuendesha shughuli zao halali za kisiasa. Acha kulalama kwa vitu ambavyo hata huvijui kwa kina.
 
Uwanja upi haupo sawa mkuu

Kwani lissu hajaruhusiwa kufanya siasa

Mbona si lipumba au Membe?
Wewe niwakusikitikiwa tu hamna namna nyingine elimu na upeo wako wa kufikiri vinahusika hapa.
 
Kiso la Magufuri ni kutoka kwao huku Burundi uhutuni kabebwa mgongoni kuja kusukumizwa na CCM kuwa rais wa kwanza mhutu Tanzania .
 
Wekeni tume huru na mazingira sawa ya ushindani wakose kitu cha kusema
 
Wa kupigwa mabomu akisalimia wafuasi wake njiani
Uwanja upi haupo sawa mkuu

Kwani lissu hajaruhusiwa kufanya siasa

Mbona si lipumba au Membe?
 
Wapi kaungwa mkono bhana msituchoshe kupinga wizi wa kura kwako ni kuunga mkono Lissu?
 
CCM wajitahidi washinde kihalali
Vinginevyo Tanzania itageuka kuwa zimbabwe.Nimefika hiyo nchi sio chini ya Mara 4 wananchi wanajutia utawala wa zanupf kwa madhila wanayopitia.Wazungu wakikuwekea vikwazo sio mchina wala mrusi anaweZa saidia.Hao watu ni namba nyingine!
 
Mkuu GUSSIE natumaini umekunywa chai vizuri.
Tukubali tukatae Mabeberu wametushika pabaya,hii ni kwasababu Serekali ilikuwa ikifanyakazi kwa nguvu badala ya kutumia akili.

Chukulia mfano suala la Korosho,nguvu ilitumika badala ya akili na maarifa.
Na hawa chomoki unawatesa watu wako hapo hapo unategemea wakusaidie kukutetea!!
 
Umesema kwa umoja wetu tutashinda, mie simo, mkisababishi vikwazo siwaungi mkononi hata kidogo!
 
Kwenye vita vya Kagera walisema Tanzania inavuruga umoja wa EA. Badala ya kumlaum Idd Amini wakaanza kumlaum mwalimu😂😂😂Hawa watu wapumbavu sana.




MAGUFULI4LIFE.
 
sirro ni mjanja ndugu natayari ameshachomoa hiyo ya kumuita asije akaleta sababu ameambiwa aendell tu na mihangaiko yake tutakutana october 28 nbaada ya uapisho wa jpm ndiyoatakapoitwa sasa akajieleze vizuri matusi yooooooooooooooooote aliyokuwa anatukana
 
Nakubalina nawe Afande Sirro IQ yake moto wa kuotea mbali - amekwisha baini mitego ya Tindu Lissu ya kuwambia tuhuma/madai yao yaorodheshwe kwenye hard copy na kuwa addressed kwa jina lake. Cha muhimu hapa Wizara ya mambo ya ndani pamoja na NEC wawe makini sana wanavyo handle masuala ya kampein wasifanye makosa ya kuonekana wana support mgombea au chama chochote - ili Lissu akose sababu/visingizio vya kusema atendewi haki - tukumbuke kwamba kujiamini kupita kiasi kwa Tindu Lissu kuna kitu, si bure. After all CCM atashinda tena safari hii come rain come shine, sasa ya nini kutaka kujiingiza kwenye mitego ya Lissu na wapambe wake. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu angependa kuona viogozi wetu wakidhalilisha kwa kuburuzwa kwenye Mahakama ya ICC the Hague - looks like Lissu and his lieutenants are overly determined that it should come to pass!! Tusiwape mwanya huo - my opinion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…