KWANINI marekebisho ya mitaala ya upili ya UK yanajenga na ya kwetu yanabomoa

KWANINI marekebisho ya mitaala ya upili ya UK yanajenga na ya kwetu yanabomoa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184









A-pupil-in-a-maths-class-009.jpg

Michael Gove said schools would want to spend more time teaching GCSE maths under the new, more demanding, curriculum. Photograph: Don Mcphee/The Guardian





New GCSE curriculum to be more demanding, says Gove

Pupils will be expected to memorise maths formulae and concentrate more on spelling, punctuation and grammar



Michael Gove said schools would want to spend more time teaching GCSE maths under the new, more demanding, curriculum. Photograph: Don Mcphee/The Guardian
The new curriculum for GCSE maths will see pupils in England spending more classtime studying the subject and memorising mathematical formulae, such as Pythagoras's theorem.
The revised maths curriculum – which comes into force in September 2015 – expands the range of topics that pupils are expected to learn, while the new curriculum for GCSE English literature and language courses will place a greater emphasis on spelling, punctuation and grammar.









UK jana nao wametangaza ukarafati mkubwa wa mitaala yao ya sekondari na kuja na vipaumbele vifuatavyo:-



1) Msisitizo wao ni kufundisha hesabu na masaa kuongezwa ila yaoane na viwango vya elimu vya mataifa yaliyoendelea duniani. Sisi hatuongelei msisitizo kwenye somo lolote ila kuridhisha wazazi ambao wako tayari kuhadaiwa ya kuwa watoto wao wamefanya vizuri huku wamefeli. Hesabu sasa UK kuongezewa mafunzo kwenye maeneo ya quadratic equations, vectors, rates of change, condition probability, n.k. Sisi kuboresha elimu hakuna uhusiano wowote na kuboresha mitaala bali kujenga mazingira ya wanafunzi kuonekana wamefaulu hata kama hawakupata ujuzi!



2) Course work assessment kufutwa UK na matokeo ya mtihani mmoja kujitosheleza kupima uwezo wa darasani wa mwanafunzi. Sisi tunawapa waalimu wajipimie maksi 40 za course work assessment ambazo hazina ukaguzi wowote ule nazo eti ziwe sehemu ya matokeo ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne! Waalimu wengi wao wanapenda kuona wanafunzi wao wakifanya vizuri hivyo kama hawawezi kuwaibia mitihani basi kazi ni moja tu…………………………kuwabandikia maksi za maendeleo ya darasani ya murua kabisa! Matokeo ya darasa la kumi sasa tutayapa asilimia 15 za matokeo ya mwisho tukisahau ya kuwa kama tumeamua kumpima mwanafunzi basi apimwe kila mwaka na chombo ambacho kiko huru na ubora wa matokeo ya shule husika.



3) Msisitizo wa UK sasa pia kuelekezwa kwenye lugha ya umombo na kushamirisha vilivyo. Sisi tunaongelea kuboresha Kiswahili kwa watoto wa wazazi wenye kipato cha chini huku wale wenye kipato cha juu wao wanaendelea kutesa kwenye mitaala ya English medium………Sijui hawa watoto mahiri kwenye Kiswahili watamudu vipi mikiki mikiki ya soko huria ambalo Kiingereza na Kifaransa ndiyo nyenzo za kutembelea.



4) UK nao wanageuza alama zao za kufaulu kutoka herufi za A* -G hadi kuwa alama za nambari za 9 badala ya A* na kushuka hadi 1 badala ya G lakini wao hawabadilishi ubora wa madaraja husika kwa maana ya viwango vya kufaulu. Sisi tunashusha ubora wa viwango vya kufaulu huku tukibadilisha daraja la sifuri kuwa tano kama vile tanzia yenye maksi chini ya 34-37 ya daraja la sifuri na kubezwa hadi kuwa daraja la tano kumeshushwa zaidi hadi kuwa chini ya maksi za kati ya 42-43 basi ni mithili ya kuvuja pakacha kuwa nafuu ya mchukuzi!

Kifupi hakuna uhusiano wowote ule katika marekebisho yetu ya uboreshaji wa matokeo ya mitihani ya upili na malengo ya kuboresha elimu bali kuwakubalia wazazi ambao wanataka watoto wao waonekane wamefaulu kumbe wamefeli………..
lengo la elimu siku zote litabakia kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa kulisukuma gurudumu la maendeleo na wala siyo hulka ya kukusanya makabrasha yenye alama za maksi za juu kama baadhi ya wanasiasa na vibaraka wao serikalini wanadhania na hata wao wamekuwa wakijirubuni na vyeti bandia kuutishia umma kuwa wamesoma kumbe ujuzi hawana hata chembe!
 
Tukubali wenzetu wametangulia na elimu yao ni bora kwani output yake tunaona wazi ktk maendeleo ya dunia.
Mimi nadhani tungefanya kama walivyofanya NBAA ambao wame review mtaala wao lakini wameitumia institute of accountancy inayoheshimika dunia nzima kwanza kureview current syllubus then kushauri mtaala mpya kuendana na dunia ya sasa hasa kuhakikisha tunakuwa na mtaala unaoweza kushindana na nchi zinazoaminika kutoa best accountants.
Mradi wa maboresho ya mtaala wa uhasibu umefadhiliwa na BOT,world bank pia.
Tunao wataalamu lakini tuwape nafasi wenzetu watupe changamoto kama njinsi mtaala wa sasa wa NBAA ulivyokosolewa na kupendekezwa mpya unaoweza kuzalisha wataalamu bora.
 
Back
Top Bottom