Kwanini matuta ya barabarani yanawekwa hata upande wa mwinuko?

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Naomba kupata elimu kwa wataalamu wa barabara TANROAD kwanini matuta yanayowekwa kudhibiti mwendo kwenye mteremko, yanawekwa hata upande wa pili wa kupanda mlima?

Nina maana kuwa bumps kama hizo ziwekwe upande mmoja tu wa kuteremka, sasa kama unamuwekea mtu anayepanda mlima, unadhibiti mwendo gani wakati kupanda kwenyewe ni mwendo mdogo?

Naomba kuelimishwa.
 
Jawabu sahihi sio kuweka bams ,maeneo yote yenye milima kwa maana ya kupandisha na kushuka ,pawed na njia mbili kila upande sio matuta
 
Kwenye kupanda Mlima kuna kuteremka pia. Umesahau hilo
 
matuta kwa sasa yamekuwa ni kero siyo nia hasa kudhibiti mwendo ni kuharibu magari tu. fikiria Morogoro pale karibu na Chuo cha kiislamu wameweka matuta 6 yale ya rasta mpaka unajiuliza ya nini kama dereva mgeni usiku unaweza mawili kuharibu gari au sababisha gari ya nyuma yako kukusukuma. Hivi mbona nchi za wenzetu hukuti matuta tena mbaya zaidi high way.
 
Umeuliza swali la msingi Sana.
Hata Mimi kuna saa Nafikiri Elimu za watu wa Tanroad Napata mashaka.
 
Kwa hiyo ulitaka waweke tuta nusu ya barabara? (Upande wa kushoto wanaoshuka). Hizo ajali zingekuwa sio za dunia hii kwani wote wanaopanda na wanaoshuka wangehamia upande usio na tuta na ajali za uso kwa uso zisingezuilika.
 
Duu! yaani mtu ahamie upande usiokuwa na tuta akate kona kurudi upande wake, ni kiwango cha juu sana za ujinga na uzembe, labda hii ni Tanzania tu. Sijui anyway
 
Kwa akili hizi za madereva wa Kiafrika, acha matuta yawekwe hata njia nzima yawe kama mataruma ya reli
 
Ha ha ha reasoning zetu balaa! Sasa ukiweka upande mmoja watu si wanapita huko kusiko na matuta? Huwajui madereva wa bongo wewe? Hujaona sehemu zenye matuta wanaweka mawe mwishoni, unajua kwanini? Watu wanakwepa hayo matuta hadi wanapita juu ya vibaraza vya watu.
NB sipendi matuta.
 
Duu! yaani mtu ahamie upande usiokuwa na tuta akate kona kurudi upande wake, ni kiwango cha juu sana za ujinga na uzembe, labda hii ni Tanzania tu. Sijui anyway
Wewe ukikuta shimo barabarani huwa hukwepi kwa kupita pasipo na shimo?
 
Tatizo hasa huku Africa madereva hawajielewi. Hivyo ina sababisha mamlaka husika zitumie theory isemayo 'Stupid actions attracts stupid reactions'. Huko ulaya mfano Germany kwenye highway, wao wanaiita 'Auto bahn' hakuna speed limit. Nyosha goti unayotaka, still Germany Auto Bahn are safest roads in Europe.
 
Duu! yaani mtu ahamie upande usiokuwa na tuta akate kona kurudi upande wake, ni kiwango cha juu sana za ujinga na uzembe, labda hii ni Tanzania tu. Sijui anyway
Umekuja lini nchini???


Hivi madereva wa bongo unawajua wewe??

Kuna hizi barabara za highways, upande wa kwenda maroli yamekandamiza hayo matuta (kutokana na uzito wa mizigo ya kwenda nchi za nje) yamepungua kidogo upande wa kushoto lakini wabongo wanakuja wanaamia hukohuko kulikokandamizwa na matter ni kushoto au kuria, kucheka, au kulia pia
 
Nchi za wenzatu zipi? Karibu kila nchi ina matuta sema Ulaya wanaweka kwenye baadhi ya barabara za mitaani. Kwa Tanzania suala la kuweka matuta mimi naliunga mkono kabisa kwa sababu madereva ni wendawazimu. Wanachotakiwa kufanya ni kuweka matuta ambao hayatasababisha uharibifu wa magari halafu yawe na alama zinazoonekana ili dereva hata akiwa mgeni ajue kuna tuta,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…