Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wewe ulitakaje?Kabla ya Mwaka 1968 Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi yenye akiba kubwa ya fedha za kigeni. Zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zilitokana na kuuza nje zao la Mkonge. Bei ya zao la mkonge lilipoporomoka na uchumi wa Tanzania nao ukatisika.
Ni kwa nini soko la ndani siyo imara sana na la kutegemeka kwa mazao ambayo tunayaita ya kibiashara? Yaani Kahawa, Korosho, Parachichi, na mazao mengine mengi,soko lake ndani ya nchi ni dogo sana chini ya asilimia tano.
Jee hali hiyo inatokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kwa watanzania kiasi cha kushindwa kununua mazao hayo au ni ukosefu wa tamaduni wa kutumia mazao hayo??
Nakubaliana na wewe kuhusu suala la Dhahabu. Kama unakumbuka baada ya Augustine Mrema kukamata dhahabu pale uwanja wa Ndege, serikali ikasema inunue yenyewe dhahabu ili kukuza akiba ya dhahabu Benki Kuu.Uchumi wa chini unakua kwa.kuuza bidhaa nje.
Kuna watu hawakuwahi kujua kama tulikuwa na Board of Internal Trade (BIT) na Board of External Trade (BET), ambazo zilishughulika na uuzaji wa mazao yetu. Lakini jee ni kwa nini BIT ilifeli kuendesha RTCs?Zamani tulikuwa na BIT na BET
Kwanza tosheleza nyumbani, halafu uwe na biashara ya kuuza nje. Tatizo letu ni umaskini. Maskini siku zote hutazama anawezaje kutoka hata kama anaishusha hadi yake mwenyewe. Ndio maana tuna shida ya chakula, mafuta ya kula, sukari n.k. nchi inaishi kwa mission town kinachoingia ndio unajua utakacho kula, hatuna maandaliziNakubaliana na wewe kuhusu suala la Dhahabu. Kama unakumbuka baada ya Augustine Mrema kukamata dhahabu pale uwanja wa Ndege, serikali ikasema inunue yenyewe dhahabu ili kukuza akiba ya dhahabu Benki Kuu.
Kilichotokea sote tunakikumbuka, Kulitokea ubadhirifu na ufujaji mkubwa wa fedha za umma kulikotokana na utapeli uliogubika zoezi zima la ununuzi wa dhahabu kupita Benki Kuu. Kwa maana nyingine hapo tena tatizo liko kwetu sisi.
Kuhusu uuzaji nje ili kukuza utajiri wetu nakubaliana na wewe, lakini jee sisi kama taifa baada ya kuuza nje ndiyo hatupati uwezo wa kununua mazao tunayoyazalisha sisi wenyewe??
Kweli kabisa, Umaskini ndiyo chanzo chake. Huwa nawauliza watu inawezekanaje kwa mama ntilie kuendelea kuuza wali kwa kati ya shilingi 1,000 hadi 1,500 kwa sahani kwenye mazingira ambapo bei za mchele na mboga anazotumia zinapanda kila siku?Kwanza tosheleza nyumbani, halafu uwe na biashara ya kuuza nje. Tatizo letu ni umaskini. Maskini siku zote hutazama anawezaje kutoka hata kama anaishusha hadi yake mwenyewe. Ndio maana tuna shida ya chakula, mafuta ya kula, sukari n.k. nchi inaishi kwa mission town kinachoingia ndio unajua utakacho kula, hatuna maandalizi
Kipato kidogo cha,mtanzania..Kabla ya Mwaka 1968 Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi yenye akiba kubwa ya fedha za kigeni. Zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zilitokana na kuuza nje zao la Mkonge. Bei ya zao la mkonge lilipoporomoka na uchumi wa Tanzania nao ukatisika.
Ni kwa nini soko la ndani siyo imara sana na la kutegemeka kwa mazao ambayo tunayaita ya kibiashara? Yaani Kahawa, Korosho, Parachichi, na mazao mengine mengi,soko lake ndani ya nchi ni dogo sana chini ya asilimia tano.
Jee hali hiyo inatokana na kutokuwa na kipato cha kutosha kwa watanzania kiasi cha kushindwa kununua mazao hayo au ni ukosefu wa tamaduni wa kutumia mazao hayo??
Nimeishia kutabasamu...Jiulize mara ya mwisho umenunua nguo lini kwa familia yako ukiacha sare za shule .