Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Ndugu Mbowe na baadhi ya vijana wake (wengi mnawaita chawa), wamekuwa hawaamini kama ndugu Lisu akishinda uenyekiti wa Chadema ataweza kuendesha chama na badala yake atakiua.
Wengine wameenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kuna uwezekano Lisu akishinda uenyekiti wa Chadema, ataanzisha siasa za uwana harakati ambao pengine utasababisha Lisu na wanaharakati wengine wa chama wakutane na kesi kama ile aliyokutana nayo Mbowe miaka kadhaa iliyopita, hivyo kupelekea chama hicho kukaa muda mrefu zaidi bila mwenyekiti wa chama taifa.
Kundi lingine linaona kwamba Lisu anaweza akakutana tena na misuko suko kama ile aliyokutana nayo baada ya uchaguzi wa 2000 ambapo ilimlazimu makamu huyo mwenyekiti wa Chadema taifa kukimbilia Ubelgiji kunusuru maisha yake, na kurudi nchini juzikati, baada ya utawala wa raisi Samia kumtaka arudi nyumban na kumhakikisha usalama wake atapokuwa nchini.
Sasa mimi sipingani na kila wanachofikiria na ukizingatia sisi ni binadam ambao hakuna anaeweza kuijua kesho yake. Sema sasa ninachoshangaa, ni kwanini ndugu Freeman Mbowe hakugombea umakamu mwenyekiti ili ilitokea kweli Lisu amefungwa au kukimbilia Ubelgiji baada ya kuwa mwenyekiti wa chama taifa, basi yeye makamu (Mbowe) akaimu nafasi yake ya uenyekiti?
Nasema hivi kwa sababu kama Mbowe angegombea umakamu basi njia ingekuwa nyeupe kwa yeye kushinda, maana hakuna ambae angekuwa na uwezo wa kumshinda kwenye nafasi hiyo.