Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Kuna hili jambo limenifikirisha sana hadi hatimaye nimepata jibu.
Ukiacha kuwa Bernard Membe alikuwa ni kama backup iwapo Tundu Lissu angeenguliwa, lakini naona kubaki kwa Membe kwenye karatasi ya kura kunaweza kuwa na faida kubwa kwa CHADEMA na Lissu siku ya upigaji kura.
Wote tunajua vita hii ya uchaguzi mwisho wake ni kwenye kituo cha kupigia kura na mawakala wa vyama na wagombea ni kiungo muhimu katika kunajisi au kupitisha matokeo halali ya kila kituo.
Sasa basi, CHADEMA wanachoweza kufanya ni kushirikiana na chama rafiki ndani ya kila kituo. Ikiwezekana CHADEMA wahakikishe wana macho 4 au hata 6 katika kila kituo.
Membe na Lissu kama wagombea wa Urais wana haki ya kuwa na mawakala katika kila kituo nchi nzima hata kule ambako wagombea wa Ubunge au Udiwani wa ACT Wazalendo na CHADEMA wameondolewa. Mawakala hawa wa ACT sasa wawe waangalizi wa ziada kwa kura za Lissu.
Lile zoezi la kuengua wagombea wa Ubunge na madiwani wa CHADEMA lilikuwa na lengo la kupunguza macho yao ndani ya vituo vya kura na hata kufifisha harakati za kampeni huko majimboni. Lakini all is not lost!
Kwa hiyo ndugu Mtanzania, usiogope wala usikate tamaa. Nenda kapige kura yako na linda kura yako kwa mujibu sheria zinavyokuruhusu. Vibaka wa kura hawana chao safari hii.