Hivi Kuna anayejua kwa nini mgeni akifika TANGANYIKA haruhusiwi kulipa Visa kwa kutumia Credit card ni hadi awe na hela Cash? Hii hulazimu wageni wasio na Visa wajazane kiwanjani wakipanga foleni kwenye ATM kupata hela za Kitanzania kwa ajili ya kulipia Visa.
Nimeandika TANGANYIKA kwa kuwa, kwa Upande wa ZANZIBAR walisha achana na huu ukiritimba siku nyingi kwa kuweka mfumo wa kupokea malipo ambao ni rafiki kwa wageni (Credit card , Cash nk)