MJ pamoja na kuwa alikuwa superstar alipenda muonekano plain , tazama hata nguo zake alizovaa, alipenda kuvaa nguo za heshima. Kuhusu sura yake; mambo mengi yalichangia (i) malezi ya wazazi hasa baba yake aliyemtesa sana wakati wa utoto, walimpiga na kumwambia mapua makubwa, hii ilimuathiri sana (kumbuka naye alipenda kuonekana vizuri mbele za watu) kisaikolojia na kuamua kufanya plastic surgery. (ii) aliwahi kupata kupata ugonjwa wa ngozi (vitiligo) uliofanya ngozi yake iwe na mabaka meupe, mabaka haya yalienea mwili mzima, ndio chanzo cha yeye kuchange ngozi (iii) aliwahi kuungua nywele akifanya tangazo la pepsi, effects ya kuungua huku ilifika hata katika sura yake hivo more plastic surgery.Pia tukumbuke watu tunazaliwa tukiwa na jinsia ya kiume ama ya kike ambazo zinakuwa supported na homoni za jinsia husika (zilizozidi zile nyingine), ila kuna watu wengine wana vichochezo ama homoni za jinsia zote zilizokalibiana japokuwa wana jinsia moja kati ya hizo, hii huathiri muonekano wa mtu, na hata sauti, ............hii inaweza kuwa ilimkuta MJ.