Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Leo nilikuwa na kazi ya kupeleka TRA maombi yangu ya kufanyiwa makadirio ya kulipa kodi maana nimefungua kampuni na wenzangu. Karatasi zangu zote zipo kamili kasoro nakala za vitambulisho vya NIDA, Afisa wa TRA akapekua akaniuliza nakala ya NIDA nikawa sina. Lakini nikajiuliza hawa hawa TRA wametupa TIN ya kampuni halafu Brela wana nakala ya vitambulisho vyetu.
Najiuliza hii mifumo yetu haisomani TRA na Brela? Mamlaka punguzeni ukiritimba dunia inatoka kutumia mikaratasi.
Badilikeni.
Najiuliza hii mifumo yetu haisomani TRA na Brela? Mamlaka punguzeni ukiritimba dunia inatoka kutumia mikaratasi.
Badilikeni.