Kwanini misemo hii ipo hivi?

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,556
Reaction score
2,571
Kuna misemo mingine mimi naona wahenga kama walikosea namna ya kuisema ili iweze kuleta mantiki katika kufikisha ujumbe husika.
mingine haikuwa na maana yoyote kuwekwa kwenye kamusi ya methali au misemo.

Kuna misemo inawafanya rika husika kuwa lazy na kutopambana kwa wakati husika, mingine imekaa kihusudahusuda na mingine imeshindwa kueleweka na jamii.

Kwa mfano eti msemo kama " vijana taifa la kesho" sikubaliani nao, kwanini vijana wasiwe taifa la leo mpaka liwe taifa la kesho. Ni nani sasa taifa la leo wazee au wakina nani?

Kuna misemo mingine ipo tu lakini wengi hawajui hata inamanisha nini kutokana na vijilugha vilivyotumika.kwa mfano kuna msemo unasema" Pema ukipemapo pema, ukipema si pema tena" ni kitu gani hiki yaani nina uhakika asilimia 90% ya watu ukiwauliza huu msemo hawaujui maana yake. So msemo utakuwa automatically umefeli kufikisha ujumbe kwa jamii.

Kuna mingine mi naona imekaa kinafiki sana na kihusuda husuda

Kwa mfano msemo unasema''Aliye juu mngoje chini''' ! Ni nini hiki ? Na kama asiposhuka je..yaani kwa lugha rahisi kwa mfano mtu kakuzidi kimaendeleo, kipesa na kilakitu kwahiyo huu msemo unamanisha umngoje chini yaani ungoje aanguke kimaendeleo jamani si utakuwa kama husuda fulani.

IPO misemo ambayo sawa ina uhalisia na inaleta mantiki kwa mfano msemo " mficha uchi hazai" hii sawa ina ukweli kabisa nakubaliana nao lakini mingine mingi yapaswa kutazamwa tena na kubadilishwa .

Ahsanteni
 
Mleta mada huenda uwezo wako wa kutafakari upo level tofauti na watoa misemo. Hakuna msemo wa "vijana ni taifa la kesho" upo wa "Watoto ni taifa la kesho".

Sula la "pema" ni mchezo wa maneno lakini wenye maana kubwa. Neno pema linamaanisha sehemu tulivu lakini katika msemo limetumika kuonesha kuchafuliwa kwa utulivu. Pema japo pema ukipema si pema tena. Kupema ni kujamba kwahiyo ni sawa na mtu akisema kuchafua hali ya hewa. Hivyo ni kweli sehemu yeyote yenye amani au utulivu ukiingiza choko choko amani hutoweka, hivyo huo msemo unamaana kubwa lakini ili kuipata maana inahitaji utulivu wa akili.

Msemo wa aliyejuu mngoje chini wengi huutumia kwenye nyanja za kiuchumi tu. Lakini katika mazingira hayo hayo ya kiuchumi msemo huu hutumiwa kama laana kwa mtu Fulani. Maneno hayo hutumiwa kwa watu ambao hutumia vipato vyao kunyanyasa wengine lakini haimaanishi kuwakatisha wengine wasitafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…