Kwanini Mishahara ya watumishi ambao wapo ngazi moja inatofautiana? Je, Utumishi huwa mnafanya kazi kisayansi kweli?

Huyo kweli mpuuzi kama ndio hivyo basi hata Halmashauri nao wangekuwa tofauti maana kuna halmashauri zina mapato kuzidi nyingine.
 
Hili linachangia sana watumishi kukataa kufanya kazi wilayani, wengi wanang'ang'ania kwenye majiji.
Nafikiri mishahara utofauti pengine ungekuwa kwenye posho na marupurupu na sio mishahara.

Lakini pia pamoja na kuwepo kwa marupurupu au posho watumishi walioko vituo vya wilayani mara nyingi hawapatiwa bali ni kuzungushwa tu tofauti na wenzao ktk vituo vingine kama MNH, NHIF nk.
 
Ndiyo maana nimesema uzoefu wangu kwa kampuni za private nilizopita...mfano wa range; utakuta grade B mshahara wake unaanzia 1M mpaka 1.5M so watu wa grade 1 wanaweza wakawa na mishahara iliyopishana kidogo
 
Nikupe zawadi gani Leo kwa pendekezo ulilotoa
 
Hii ndio tafsiri rahisi ya 'divide and rule', watanzania kamwe hatuwezi kuwa wamoja na kupambania haki zetu maana tumeshawekwa kwenye madaraja tofauti tofauti na watawala wa kijani.

Hii nchi pamoja na mazuri machache, mambo ya ovyo ni mengi zaidi. Mojawapo ndio hilo la watumishi wenye elimu sawa, kada sawa na daraja sawa kupewa mishahara tofauti tofauti.
 
Wizo una suti mpya? 😹
 
Haipaswi kuwa hivo
Mimi na ww tumesoma marketing chuo kimoja tunmemaliza mwaka mmojq. Pengine hata GPA zinafanana lakini ukienda NIMR na Mimi nikienda Halmshauri, wewe utakuwa na Mshahara mkubwa kuliko Mimi with henefits .

Kosa langu mm ni kwenda Halmashauri kuhudumia wananchi. Haipaswi kuwa hivi
Umeelewa……wote ni watumishi
Standardization ni muhimu
 
Nimeipenda hii comment ni ya kitaalamu lakini inaeleweka hata kwa sisi ngumbaru
 
Nimeipenda hii comment ni ya kitaalamu lakini inaeleweka hata kwa sisi ngumbaru
 
Nimeipenda hii comment ni ya kitaalamu lakini inaeleweka hata kwa sisi ngumbaru
Serikali ndio source ya mambo haya ya hovyo.
Unakuwa mshahara wa watumishi 2 wenye sifa sawa unatofautiana zaidi ya mara mbili au tatu eti kwakuwa mwingine yuko kwenye shirika la umma na mwingine anatoa huduma kama afisa mtendaji wa kata. Shirika lenyewe consuming iko juu kuliko production
 
Mkuu jibu ni hili...

Ni kweli wote wamemaliza mwaka mmoja, level moja, na Chuo kimoja lakini tofauti inakuja kwenye uwezo hawawezi wakawa na uwezo sawa lazima watofautiane...

Sasa wanajuaje huyu anauwezo kushinda mwingine, hapo sasa ndio linakuja suala la qualifications ume-performance vipi.

Hapo ndipo tofauti inaanza una GPA ya ngapi? Na katika interview ya kazi hiyo uli-perform kiwango gani uhusiano utakaopatikana hapo ndio utaamua upangwe wapi!

Kama GPA ni ndogo na katika usahili performance ni yakawaida basi unajikuta upo wilayani huko(HALMASHAURI).

Na kama GPA ni kubwa na ukaperform vizuri katika usaili wa hiyo kazi/nafasi basi unajikuta katika Taasisi na wizarani huko.

Haya ni mawazo yangu mkuu hembu jaribu kuichunguza na wewe.
 
Mkuu jibu ni hili...

Ni kweli wote wamemaliza mwaka mmoja, level moja, na Chuo kimoja lakini tofauti inakuja kwenye uwezo hawawezi wakawa na uwezo sawa lazima watofautiane...

Sasa wanajuaje huyu anauwezo kushinda mwingine, hapo sasa ndio linakuja suala la qualifications ume-performance vipi.

Hapo ndipo tofauti inaanza una GPA ya ngapi? Na katika interview ya kazi hiyo uli-perform kiwango gani uhusiano utakaopatikana hapo ndio utaamua upangwe wapi!

Kama GPA ni ndogo na katika usahili performance ni yakawaida basi unajikuta upo wilayani huko(HALMASHAURI).

Na kama GPA ni kubwa na ukaperform vizuri katika usaili wa hiyo kazi/nafasibasi unajikuta katika Taasisi na wizarani huko.

Haya ni mawazo yangu mkuu hembu jaribu kuichunguza na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…