Kwanini Mji wa Jerusalem ni Mtakatifu?!

Kwanini Mji wa Jerusalem ni Mtakatifu?!

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Kumekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Mji huo kwa sasa huwa umegawanywa mara mbili, Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.

Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu nayo Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa), ingawa eneo hilo bado kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya 1967.

Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa. Eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000.

Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikubali azimio hilo.

Hivyo basi, balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Jerusalem, katika mji wa Tel Aviv.

Mzozo huo umefufuliwa tena kutokana na hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kutarajiwa kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Mataifa mengi ya Kiarabu yameshutumu hatua hiyo ya Bw Trump na kusema itazidisha uhasama Mashariki ya Kati

Dini tatu

Mji huu huwa na umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu - Ukristo, Uislamu na Uyahudi. Dini zote tatu humuangazia Abraham anayetajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani.

Ni mji ambao umedhibitiwa na dini hizo kwa vipindi mbalimbali katika historia.


Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu. Mji huo ni miongoni mwa miji ya kale zaidi ambayo ipo hadi sasa duniani.

Ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kisha kujengwa tena.

Kila sehemu ya ardhi yake ukichimba kwenda chini hufichua enzi fulani katika historia yake.

Ingawa umekuwa chanzo cha ubishi na mzozano kati ya dini mbalimbali, dini zote huungana kwa pamoja kuungama kwamba ni eneo takatifu.

Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia. Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.

Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.

Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia

Kanisa

Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa Yesu Kristo, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.

Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Yesu.

Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.

Kanisa takatifu lafunguliwa Israel
Chumba alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel
Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.

Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.

Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.

Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.


Msikiti

Mtaa wa Waislamu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.

Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf.

Waislamu huamini kwamba Mtume Muhammad alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote. Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe la msingi. Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.

Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.


Ukuta

Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka lililokuwa Hekalu Takatifu.

Ndani ya hetalu hilo kulikuwa na Patakatifu pa Patakatifu, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.

Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa.

Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac. Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa patakatifu

Husimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji.

Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia hutembelea eneo hilo kuomba na kukumbuka utamaduni wao, hasa nyakati za siku kuu za kidini.

Ukuta huo pia hufahamika kama Ukuta wa Maombolezo.
175d061495febfbfeeae2aed60d2e121.jpg
 
Wote ni wayahudi
Tofauti yao ni kuna mafarisayo, masadukayo, waislam, wakristo

Nomba nikurekebishe hapo kwenye bold. Hakuna Myahudi Mkristo wala Muislamu. Isipokuwa kuna Waisraeli Wakristo, Waislamu na Wayahudi. Uyahudi ni dini, siyo utaifa. hata wewe mwafrika unaweza kuwa Myahudi kama ambavyo unaweza kuwa Mkristo au Muislamu au dinio nyingine yeyote ile. Isipokuwa miongoni mwa Wayahudi kuna Marafisayo na Masadukayo.
 
Mleta uzi acha upotoshaji na bulaabula bana.. Mungu ana mpango wake maalamu kwa mwanadamu. Yaani mpango wa kumkomboa mwanadamu kutoka laana ya dhambi iliyofanywa pale Eden na Adam na Hawa baada ya kudanganywa na shetani/ nyoka. Na huu mpango uko katika mlolongo huu ufuatao; Ibrahim akaja Isack akaja Yakobo/Israel akaja Daudi akaja Bwana Yesu/Mungu aliye uvaa uwanadamu/Emanueli, "Mungu pamoja nasi". Tofauti au nje ya hapa/hapo ni mpango wa shetani.

Hebu niambie lile hekalu la Mungu ambalo alimuambia mtumishi wake Daudi amjengee na baada ya majukumu ya Daudi ya vita kuikomboa kaanani nchi ya ahadi kwa kuwapokonya wafilisti/wapalestina kumzidia, ikabid Mungu akasimishe jukumu hili kwa mwanae na mrithi wake mfalme Sulemani/Solomoni. Je hekalu hili liilikuwa katika eneo gani kati ya haya ulio ya ainisha hapa katika huu uzi wako? Msipotoshe ukweli na historia kwa manufaa ya shetani/nyoka.

Tabia ya shetani/joka tangu pale bustani ya Eden iko hivi, kujichanganya katika mpango wa Mungu kwa wanadamu na kuuvuruga. Alimlaghai Hawa na hatimaye Hawa akamshawishi Adam na wakatenda dhambi ya kumkaidi Mungu na kula liletunda la mti wa katikati ya bustani walilo kuwa wamekatazwa wakaanguka dhambini kwa huko kutokumtii Bwana Mungu wao.

Hivyo hivyo wakati wa Ayubu ikatokea viumbe wa mbinguni/malaika/heavenly beings wamekusanyika na shetani akajichanganya kati yao. Ikabidi Mungu amulize "shetani unatokea wapi na unaenda wapi?" Na baada ya hapo kilicho mpata Ayubu chajulikana.

Lakini hata hapo nchi ya ahadi ya kaanani uliko mji wa Yerushalaymi, ambayo Ibrahim" Baba wa imani" kwa kupitia uzao wake kwa Yakobo/Israel alipewa na Mungu kwa matakwa na mapenzi ya Mungu ili kuirithi. Ambayo hamna mwanadamu ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu, Mungu mmoja nawakweli anaye weza kuyahoji, napo shetani kwa kupitia wafuasi wake amejichanganya na anaendeleza juhudi zake za uharibifu kwa kupavuruga na kupanajisi.

Mfano halisi ni huu uzi hapa. Mtu kama huyu mleta maada inawezekana vipi asijue ukweli kuhusu Hekalu la Mungu ambalo lilijengwa katika hili eneo analolizungumzia?

Kuwa hili hekalu ni la Wayahudi na lilijengwa na mrithi na mwana wa mtumishi wa Mungu mfalme/nabii Daudi yaani Mtumishi wa Bwana Mungu wa Majeshi mfalme Suleiman/Solomon. Mtu anaye sifika na kujulikana ulimwenguni kote/pote kwa karama ya hekima aliyokuwa amejaaliwa/kukirimiwa na Mwenyezi Mungu.

Kuwa hili hekalu lilikuwa ni la Wana wa Israel/Wayahudi na ndipo walipo kuwa wanamfanyia Mwenyezi Mungu ibada zao na kumtolea sadaka za kuteketezwa.

Kuwa ndiko kuliko kuwa kumehifadhiwa lile sanduku la Agano la Mungu na wana wa Israel alilo pewa Musa na lililopewa jina la "Bwana Mungu wa Majeshi" Na hili hekalu lilitabiriwa na manabii tangu enzi na enzi kuwa lingevunjwa na kuharibiwa na wafuasi wa Ibilisi katika zama tofauti tofauti. Na hivyohivyo litakuwa baada ya kuvunjwa/kuharibiwa na hao wafuasi washetani na kumilikiwa nao kwa hizo zama, hivyo hivyo litakuwa linakombolewa na watumishi wa Mungu watakao kuwa wananyanyuliwa katika zama/nyakati tofauti tofauti

Ni ukweli ulio wazi kuwa eneo lilipokuwa hili Hekalu la Mwenyezi Mungu kwa wakati huu wa sasa halimikikiwi/haliendeshwi/kuhudumiwa na wana Waisrael na wanao abudu katika eneo hilo sio Wayahudi na lazima tunapoelekea ule mwisho wa Dunia yaani kuelekea kurudi kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu/ Mungu hapa duniani lazima eneo hilo likombolewa kutoka kwa wamiliki wake wa sasa na Hekalu lijengwe upya/restored. Na hapo ndipo kiini cha mgogoro/ugomvi huwa wa sasa kilipo. Kuwa shetani kwa kupitia wafuasi wake kangangania eneo lilipokuwa hekalu la Bwana Mungu wa Majeshi, period!!!
 
Wote ni wayahudi
Tofauti yao ni kuna mafarisayo, masadukayo, waislam, wakristo

Point of corrections mafarisayo/walimu wa sheria, masadukayo/hawa tunaowaita siasa kali siku hizi au extrimists. Na hawa waweza kuwa Wayahudi au Wakristo au Waislamu au Masingasinga nk,nk,nk....
 
Back
Top Bottom