NIPASHE
2008-02-28 10:39:19
Na Joseph Mwendapole
Kuhusu tuhuma kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, alifanya biashara akiwa Ikulu, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ilisema haitamchunguza Mkapa kwa kuwa hawajapata malalamiko yoyote.
Ofisa Habari wa Sekretarieti hiyo, Bw. Augustus Karia, alisema hawawezi kufanya uchunguzi kwa maneno ya kusikia mitaani.
``Sheria iko wazi na nendeni mkasome, sisi hatuwezi kuchukua hatua hewani lazima kuwe na mtu ambaye amekuja ofisini kwetu kulalamika,``alisema.
Jitihada za kuonana na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji Steven Ihema, kwa ufafanuzi zaidi zilishindikana baada ya kukataa kuzungumza na waandishi.
Chanzo: NIPASHE, Alhamishi 28 Feb.2008
SABABU ZA KUTOKAMATWA KWA MKAPA HIZO HAPO JUU kwee kwee kweee, hii Tanzania.....