Kwanini mnaibeza kauli ya Rais ya jana

Trump ye ni mfanyabiashara ye amepata soko kwetu. Na hivo lazima atupongeze na atsifie ili biashara kati yetu iendelee sa kuja kutangaza huk kua umepongezwa na muuzaji wa bidhaa ni ushamba tu.
Ila Mkuu Trump angetukosoa kwa kununua Ndege wakati s kipaumbele sana kama wengine wanavyosema si kauli yake msingeitumia
 
Wengi mwadhani kukumbukwa tu jina lako na Trump ni mchezo. Weye kakutamka mara ngapi?? Acha tujisifu kwa kuwa sasa hata katika meza za chakula huko kwa wakubwa wanaweza kulitamka vizuri sasa jina la nchi yetu zuri
 
Je Ukienda dukani kununua mabati, mwenye duka akakusifu kwa kununua mabati utaenda kutangaza kitaa kuwa nimenunua mabati hadi mwenye duka kanisifu?
Lakini inaonesha muuzaji anakukubali unatoa pesa kamili si longolongo
 
Mzee bwana yani basi tu.
Tumshukuru Mungu hata kwa huyu maana ni somo tunapitia.
Tutanunua ndege nyingine nyingi tu kwa kuwa TRUMP anatupongeza, halafu tukifilisika Trump atasema look the shitholes!
 
Ukinunua cocaine kwa muuza cocaine, halafu muuza cocaine akakupongeza kwa kununua cocaine, umekuwa "mteja" mara mbili.

Mteja kwa kuwa mnunuzi, mteja kwa kuwa mtumia madawa ya kulevya.

Kufurahia muuza cocaine kukusifia ununuzi ni ulimbukeni.

Sasa ulitegemea muuza cocaine asifurahi ukinunua cocaine kwake?

Marekani inafurahia watu kununua hata silaha kwake, sasa Mmarekani akifurahi usifikiri hicho ni kitu kizuri kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…